Home Kimataifa DAVID DE GEA HUYOOO KUELEKEA REAL MADRID.

DAVID DE GEA HUYOOO KUELEKEA REAL MADRID.

868
0
SHARE

de gea

David De Gea ni mzaliwa wa Madrid na ameanza kucheza soka akiwa na Atletico Madrid na baadae kutimkia Man United. Kuna uwezekano kwamba De Gea akarudi kwenye jiji alilozaliwa ambako kuna club kubwa inamuhitaji ambayo ni Real Madrid.

Sio siri kwamba golikipa wa Manchester United anatakiwa sana na Real Madrid, mtangazaji wa kipindi maarufu cha mambo ya michezo huko Hispania amesema kwamba David De Gea amesema yes, yupo tayari kwa Real Madrid msimu ujao.

Mtangazaji huyo amesema kwamba amezipata hizo habari na kusema kwamba “Kipa wa Manchester United anataka kuvaa jezi nyeupe ya Real msimu ujao. Club ya Real imezingatia mambo mengi kwenye swala la ulinzi wa goli lao na wameamua kwa De Gea.”

Aliongezea kwamba,”Na De Gea yupo wazi anataka kulinda lango la Real Madrid kuanzia msimu ujao”.

Uhamisho wa wachezaji wa kutoka Manchester United kwenda Real ni kitu cha kawaida na kinachowezekana kwasababu wachezaji wakubwa kama Cristiano Ronaldo, David Beckham wote walipitia njia moja.

De Gea ana miaka 24, urefu wa 6.4 ft na Real Madrid inaweza kuwa club yake ya 3 baada ya Atletico na Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here