Home Kitaifa ulio aja na visingizio akifungwa Taifa leo

ulio aja na visingizio akifungwa Taifa leo

703
1
SHARE

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
‘Coastal ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Februari 4, mwaka huu.’

MECHI ya Yanga SC dhidi ya Coastal Union FC Uwanja wa Taifa jijini hapa leo, imesababisha mgogoro kati ya kocha mkuu wa Wagosi wa Kaya hao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na uongozi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara 1998, imeelezwa.
JULIO
Katika kile kinachoonekana kama kuweka tahadhari endapo kikosi chake kitapata matokeo mabaovu dhidi ya Yanga SC leo, Julio ameweka wazi kuwa kumetokea msuguano kati yake na uongozi wa Coastal Union kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba ya ligi hiyo msimu huu yaliyoigusa pia mechi hiyo Na. 157.

“Ratiba yenyewe nimejua juzi saa tatu asubuhi kwamba tutacheza dhidi ya Yanga Jumatano (leo). Nimegombana na uongozi kwa sababu baada ya mechi ya Jumamosi niliwapa mapumziko wachezaji nikijua mechi iko tarehe 18 ya mwezi huu,” Julio amesema.

“Kama unavyowajua wachezaji wa Kitanzania ukishawapa likizo wanakula kila kitu. Wameenda kukutana na wanawake zao huko, unatarajia nini uwanjani?

“Lakini, kwa kuwa sisi ni wanajeshi, tunapeleka timu uwanjani leo na ninaamini itafanya vizuri. Kila mchezaji yuko vizuri kiafya, ni juu yangu kuchagua wepi wa kuwatumia na kutowatumia.”

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Simba SC, hakuwa tayari kuweka wazi mahali kilipo kikosi chake kikisubiri kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga SC katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Februari 4, mwaka huu.

Kwa upande wao Yanga SC kupitia kwa kocha msaidizi wa Yanga SC , Boniface Mkwasa, wametamba kufanya kweli dhidi ya Coastal leo.

Aidha, Mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga, Jerry Muro, amesema jijini hapa leo kuwa kikosi chao kiliingia kambini jijini jana asubuhi kwa ajili ya mechi hiyo.

“Wachezaji wetu wote wako fiti, isipokuwa (Andrey) Coutinho ambaye huenda akaanza kucheza dhidi ya Mbeya City Jumapili,” amesema Muro.

Coastal Union FC, iliishika Yanga kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa msimu uliopita, mechi ambayo ilimponza refa bora wa VPL 2011/12, Martin Saanya, ambaye alifungiwa msimu mzima kwa madai ya kuibeba timu hiyo ya Tanga kwa kuipa tuta dakika ya mwisho.

Kikosi cha Julio ambacho kiko hatarini kuporomoka daraja msimu huu, kitakuwa na mtihani mgumu mbele ya vinara hao wa msimamo ambao hawajawahi kufungwa na timu nyingine ya ligi kuu ya Bara Uwanja wa Taifa msimu huu mbali na Simba SC na Azam FC.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here