Home Kitaifa Mabondia Julius, Saidi Uwezo kuchapana march 28

Mabondia Julius, Saidi Uwezo kuchapana march 28

540
0
SHARE

11073562_836973369682141_7670068943810083201_nNa Mwandishi Wetu
Mabondia Julius Kisarawe kutoka ‘Ndame Club’ na Saidi Uwezo kutoka ‘Mzazi GYM’ watapanda uringoni march 28, kugombania ubingwa wa Taifa wa kg 54, katika ukumbi wa manyara park, uliopo CCM Tandale, Manzese.

Mpambano huo wa raundi kumi wenye upinzani wa hali ya juu utasindikizwa na mabondia mbalimbali kutoka katika kambi tofauti.

Bondia Ibrahimu Tamba, atapambana na George Dimoso huku Vicent Mbilinyo kutoka kwa ‘Super D Boxing Coach’ atapambana na Yusufu Mkari, Kasimu Gamboo atakabiliana na Mustafa Dotto alafu Mohamed Kibanga atapambana na Bakari Dunda wakati Karim Mura atamkabili Eddy Baguo.

Siku hiyo kutakuwa na uuzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali.

DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, ambapo alisema kuwa DVD hizo ni kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here