Home Kitaifa Dakika 45 za kwanza zakatika Yanga 2 Platinum Stars 1

Dakika 45 za kwanza zakatika Yanga 2 Platinum Stars 1

518
0
SHARE

NIYONZIMANEW4Na, Richard Bakana, Dar es Salaam

Dakika 45 za kwanza za mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya wenyeji Yanga SC pamoja na Platinum Stars ya Zimbabwe, zimemalizika huku Watanzania hao (Yanga SC) wakiwa mbele kwa bao 2-1.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Salum Telela katika dakika ya 28 pamoja na Haruna Niyonzima dakika ya 44, zikiwa zimebakia sekunde chache ili mwamuzi aweze kupuliza kipenga kuashiria dakika 45 za kwanza kumalizika, Platinum Stars waliweza kusawazisha kufatia mpira wa adhabu ndogo ambapo ulipigwa na kuingia langoni moja kwa moja.

Katika kipindi cha kwanza Yanga watajutia sana nafasi ambazo wamezipoteza kwani washambuliaji wake, Simon Msuva, Ngassa na Tambwe leo wameongoza kwa kukosa mabao ya wazi, kitu ambacho kingewafanya warejee kwenye vyumba wakiwa mbele kwa zaidi ya bao 3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here