Home Kitaifa YANGA WATANGAZA KUNYAKUA UBINGWA, WAAHIDI DOZI KWA ATAKAYEKATIZA MBELE YAO

YANGA WATANGAZA KUNYAKUA UBINGWA, WAAHIDI DOZI KWA ATAKAYEKATIZA MBELE YAO

763
0
SHARE

DSC_0276

Mshambulaiji wa Yanga, Amissi Tambwe akijaribu kumfunga kipa wa Mtibwa, Said Mohammed walipokutana jana katika mechi ya ligi kuu uwanja wa Taifa Dar es salaam, Yanga ikishinda 2-0.

Na Richard Bakana, Dar es salaam

 MABINGWA wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans (Yanga SC) jana wametangaza rasmi kuusaka ubingwa wa ligi hiyo unaoshikiliwa na Azam FC baada ya kuwapokonya mwaka jana.
Akizungumza na Shaffihdauda.com Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema kuwa walikuwa wakienda kimya kimya lakini kufuatia ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Taifa sasa wameamua kuweka hadharani kuwa ubingwa wa VPL msimu wa 2014/2015 lazima utue Jangwani.
“Kwa ujasiri na Madaraka niliyonayo napenda kuwatangazia wanachama wa Yanga kuwa leo (jana) tumeanza rasmi kusaka ubingwa wa ligi, timu yoyote inayojua itakutana na Yanga basi wajiandae kwa kipigo” Amesema Jerry ambaye alitua Jangwani akichukua mikoba ya Baraka Kizuguto.
Jerry amesema kuwa mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar ulikuwa ni kipimo kizuri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho hapo wiki kesho ambapo watakuwa wenyeji wa klabu ya BDF kutoka Botswana huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuipa nguvu timu yao pindi inapokuwa Uwanjani.
“Sisi tumeanza kujiandaa kwa mwezi mzima, Mtibwa ndio ilikuwa kipimo chetu na sasa tuko tayari” Ameongezea Jerry.
Jana jioni Yanga ilikutana na Mtibwa katika Uwanja wa Taifa na kufanikuwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 magoli yaliyotupiwa kambani na Mrisho Ngassa na kurudisha matumaini ya kupangwa katika kikosi cha kwanza chini ya Kocha Hans Van De Pluijm.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here