Home Kitaifa AZAM WAINGIA KWA TAHADHARI KUWAVAA STAND UNITED LEO

AZAM WAINGIA KWA TAHADHARI KUWAVAA STAND UNITED LEO

301
0
SHARE

??????????

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaingia kwa tahadhari kubwa katika mechi ya leo ya ligi kuu itayopigwa uwanja wa CCM Kambarage Mkoani Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand United.

Meneja wa Azam fc, Jemedari Said Mzumari amesema wanaingia uwanjani wakitambua wanacheza na moja ya timu 14 zinazogombea ubingwa wa VPL.

“ Stand United ni moja ya timu nzuri ambazo zilianza ligi kwa kusuasua, lakini zikapata kasi wakati ligi inaendelea” Alisema Jemedari. “ Mechi nyingi tu wamepata matokeo mazuri, walipata matokeo mazuri dhidi ya Simba uwanja wa Taifa, wamepata matokea ugenini dhidi ya viongozi wa ligi ambao hawajafungwa Mtibwa Sugar”

“Pia Bukoba walipata matokeo mazuri, hii inaonesha kwamba ni timu inayobadilika na kadri siku zinavyokwenda inazidi kuimarika, isipokuwa sisi kama mabingwa watetezi wa kombe hili, tunaamini kuwa sisi ni timu yenye mchanganyiko mzuri wa wachezaji katika ligi hii na ni timu imara, tumepania kupata pointi tatu na si tatu tu, bali ni tisa katika michezo mitatu kabla hatujasafiri kwenda Lubumbashi”.

“Tumejiandaa leo kupata pointi tatu, halafu tutakwenda Mwanza kuchukua pointi tatu kabla ya kukwaana na Simba Dar es salaam”. Amesema Jemedari.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here