Home Kitaifa MKUDE AZIPA TANO MBINU ZA KOPUNOVIC

MKUDE AZIPA TANO MBINU ZA KOPUNOVIC

515
0
SHARE

???????????????????????????????

KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Gerrard Mkude amesema kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi ni mwanzo mzuri wa kufanya vizuri katika mechi za ligi kuu Tanzania bara.

Mkude ameuambia mtandao huu kuwa kocha Goran Kopumovic amekuja na mbinu mpya ambazo zinawasaidia kuwa imara.

“Kocha anataka kushambulia kwa kasi na kukaba sana. Ni mwalimu mzuri. Ujue kila mwalimu ana ubora wake. Hata Phiri (Patrick) alikuwa mzuri, sema kuna kutofautiana”.

Kiungo huyo tegemeao alisema mafanikio ya ubingwa wa Mapinduzi ni umoja na mshikamano kwa wachezaji wote wa Simba, mashabiki na viongozi.

“Mechi haikuwa rahisi, lakini tulijituma kwa dakika zote na hatimaye tumevuna matokeo mazuri”. Alisema Mkude.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here