Home Kitaifa SIMBA, MTIBWA SUGAR ZAKUTANA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

SIMBA, MTIBWA SUGAR ZAKUTANA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

773
0
SHARE

IMG_4303

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wametinga fainali ya kombe la Mapinduzi kufuatia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Polisi katika mechi wa nusu fainali ya kombe hilo iliyomalizika usiku huu uwanja wa Amaan Zanzibar.

Bao pekee la ushindi limefungwa katika dakika ya 36 kupitia kwa winga Ramadhan Singano ‘Messi’ akizamisha moja kwa moja mpira wa adhabu ndogo.

Simba na Mtibwa Sugar zitachuana katika mechi ya fainali itakayopigwa uwanja wa Amaan Januari 13 mwaka huu.

Simba waliuanza mpira kwa kasi wakipiga mpira wao wa pasi, lakini mipango iliharibika upande wa kulia kwani beki anayepandisha mashambulizi Hassan Ramadhan Kessy alipoteza pasi kadhaa alizopewa na Saimon Sserunkuma.

Safu ya ulinzi ya Simba ikiongozwa na Hassan Isihaka na Juuko Mursheed katika dakika 10 za mwanzo haikuwa na utulivu wa kutosha kwani mabeki walichanganyana  mara kwa mara na washambulizi wa Polisi wangekuwa makini wangefumania nyavu.

Simba waliendelea kufika eneo la wapinzani wao na katika dakika ya 17 na 18, Kiungo Said Hamis Ndemla alipiga mashuti makali takribani mita 24 kutoka golini, lakini mlinda mlango wa Polisi, Suleiman Mzee alifanya kazi nzuri na kuokoa hatari hizo.

IMG_4270

Katika dakika ya 26 winga wa kulia wa Simba, Saimon Sserunkuma alimhadaa beki wa Polisi, Steven Mayala karibu na eneo la kibendera cha kona, lakini beki huyo alimzuia na mwamuzi akaamuru mpira wa adhabu ndogo.

Ramadhan Singano ‘Messi’ alikwenda kupiga mpira huo na ‘guu’ lake la kushoto na gozi la ng’ombe likazama moja kwa moja nyavuni huku kipa Mzee akiambulia patupu.

Hilo lilikuwa bao la pili kwa Singano kwani alifunga pia Simba ikishinda bao 1-0 dhidi ya JKU katika mchezo wa mwisho wa kundi C.

IMG_4274

Dakika ya 36, Singano aliingiza krosi murua, almanusura Saimon acheke na nyavu isingekuwa jitihada za golikipa mzee.

Simba waliendelea kulishambulia lango la Polisi kama nyuki na katika dakika ya 45, Kessy alimpiga mpira mrefu winga ya kushoto na kumkuta Danny Sserunkuma aliyemiliki gozi na kupiga pasi nzuri ndani ya eneo la sita, lakini beki Daniel Joram wa Polisi aliondoa mpira huo na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Simba wanaonolewa na Mserbia Goran Kopunovic walitoka kifua mbele kwa bao 1-0.

Kwa ujumla katika kipindi hicho, Simba walicheza mpira mzuri wakimiliki kwa asilimia 60 dhidi ya 40 za Polisi.

Winga wa kulia Simon Sserunkuma alikuwa mwiba mkali kwani alionesha kiwango kikubwa akipiga pasi safi, chenga za uhakika na krosi kadhaa.

Tatizo la Simba katika kipindi cha kwanza lilionekana safu ya ulinzi ambapo Mursheed na Isihaka hawakuwa na uelewano mzuri. Pia Mohammed Hussein na Kessy walifanya makosa mara kwa mara.

Ingawa Polisi walizidiwa kwa vitu vingi, walijitahidi kushambulia kwa kushitukiza, lakini Mlinda mlango Peter Manyika alifuta makosa ya mabeki wake kwa kuokoa mipira ya hatari.

Dakika ya 45, Simba walifanya mabadiliko ambapo Elius Maguli akwenda benchi na nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Hajibu ‘Mido’.

Dakika ya 46, Danny Sserunkuma alipata nafasi nzuri baada ya kubaki yeye na golikipa, lakini alishindwa kufumania nyavu akipiga mpira uliodakwa na kipa Mzee.

Katika dakika ya 47 Polisi nao walimtoa Adam Juma na nafasi yake ikachukuliwa na Rashid Jumanne.

Dakika ya 56 Polisi walifanya mabadiliko wakimtoa Abdallah Omary na nafasi yake ikachukuliwa na Mohammed Seif.

Dakika ya 58 Polisi walifanya mabadiliko tena wakimtoa Samir Vicent na nafasi yake ikachukuliwa na Steven Emmanuel.

Dakika ya 60 Polisi walipata kona, lakini haikuzaa matunda baada ya kipa Manyika kuudaka mpira huo.

Dakika ya 61 Danny Sserunkuma alipata nafasi nyingine na kupiga shuti ambalo halikulenga lango.

Simba walifanya mabadiliko katika dakika ya wakimtoa Singano na kumuingiza Shaaban Kisiga ‘Malone’.

Dakika ya 68 Hajibu alipiga shuti kali kufuatia kupokea pasi ya Mursheed, lakini kipa Mzee alikoa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Nyota huyo aliyefunga ‘hat-trick’ katika ushindi wa Simba  wa 4-0 robo fainali dhidi ya Taifa ya Jang’ombe alipata nafasi ya kutoa pasi kwa Danny, lakini akalazimisha kupiga shuti ambalo lilikuwa mboga kwa kipa.

Simba walifanya mabadiliko tena katika dakika ya 79 wakimtoa Simon na kumuingiza Awadh Issa Juma.

Wakati huo huo kamati ya mashindano ya kombe la Mapinduzi imemtangaza Said Ndemla kuwa mchezaji bora wa mechi na amekabidhiwa zawadi ya king’amuzi cha Azam TV

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here