Home Uncategorized QUEIROZ AMKANA FERGIE KWENYE UHAMISHO WA BEBE

QUEIROZ AMKANA FERGIE KWENYE UHAMISHO WA BEBE

728
0
SHARE

IMG_8699.JPG

Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Carlos Queiroz amesisitiza kwamba hakuhusika na kwa na jambo lolote kwenye uhamisho wa £7.4 million uliomleta mchezaji Bebe Old Trafford.

Bebe alijiunga na Vitoria de Guimaraes lakini Sir Alex Ferguson alikiri hakuwahi kumuona mchezaji huyo akicheza soka na usajili wake uliamuliwa kwa ripoti ya skauti na mazungumzo na Queiroz.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 aliwahi kuichezea 2 mbili tu za mashindano kabla ya uhamisho wake wa kwenda Benfica kwa ada ya uhamisho £2.3m mwezi July na Queiroz, ambaye alikuwa kocha wa Ureno wakati wa uhamisho wa Bebe mwaka 2010, anasisitoza kwamba hakujua chochote kuhusu mshambuliaji huyo.

“Bebe hakuwa hata kwenye sehemu ya mafaili ya skauti ya timu ya taifa ya Ureno,” Queiroz aliliambia jarida la FourFourTwo.

“Hakuwepo kwenye mfumo ambapo tulikuwa na kila data ambazo zilikuwa na taarifa za wachezaji wote. Hivyo Bebe kwenda Man United ni jambo lilonishtua.

“Niliwapigia makocha na kuwauliza nini kilikuwa kinaendelea, kwanini hakuwa kwenye data zetu. Sikuwa najua chochote kumhusu mchezaji huyo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here