Home Kimataifa DAVID JAMES AFILISIKA – AANZA KUPIGA MNADA MALI ZAKE

DAVID JAMES AFILISIKA – AANZA KUPIGA MNADA MALI ZAKE

1145
0
SHARE

Golikipa wa zamani wa England David James ameamua kufanya mnada wa vitu vyake kama jezi zilizosainiwa, mipira ya mechi alizowahi kucheza baada ya kufilisiwa mwezi Mei mwaka huu.

Golikipa ambaye ana rekodi ya kucheza mechi nyingi katika ligi kuu ya England David James, ambaye hivi karibuni alirudi kucheza soka baada ya kustaafu – akienda kujiunga na Indian Super League kwenye timu ya Kerala Blasters FC, amekuwa akiandamwa na madeni mengi baada ya kuachana na mkewe mnamo mwaka 2005.

1415176686052_wps_12_image001_png
Mchezaji huyo mwenye miaka 44, amewahi kuvichezea vilabu vya Liverpool, Manchester City na Portsmouth wakati alipokuwa akicheza soka la ushindani, anatajwa kuupoteza utajiri unaofikiwa £20million.

James ameamua kuuza zaidi ya vitu 150 kupitia mtandao wa Hilco.
Watu sasa watakuwa na uwezo wa kutoa ofa ya kununua vitu hivyo, kuanzia November 6-18.

article-2820886-22DBC0A700000578-949_636x471 1415175031463_wps_10_James_Auction_DONE_jpg

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here