Home Kimataifa BAADA YA LIVERPOOL KUCHEZESHA RESERVES SABA JANA USIKU – JE WAMEVUNJA SHERIA...

BAADA YA LIVERPOOL KUCHEZESHA RESERVES SABA JANA USIKU – JE WAMEVUNJA SHERIA NA WATAADHIBIWA NA UEFA?

1326
0
SHARE

Baada ya jana usiku kutangazwa kwa kikosi cha Liverpool ambacho kilishuka dimbani kucheza na Real Madrid kulianza maneno maneno ya uchaguzi wa wachezaji aliofanya kocha Brendan Rogers.

Dhidi ya klabu bora zaidi duniani kwa sasa, Rodgers akaichagua timu ambayo iliundwa na wachezaji wengi wa kikosi cha pili, akifanya mabadiliko saba kutoka kwenye mechi yao ya wiki mbili zilizopita, jambo ambalo liliamsha mjadala mkubwa miongoni mwa wapenzi wa soka duniani.

Katika moja ya hoja zilizotolewa kwenye mjadala wa kikosi cha Liverpool jana ni jambo la kisheria ambapo kwa mujibu wa Sheria za UEFA, kuna sheria inayowalazimisha vilabu kuchezesha vikosi vyao imara zaidi katika muda wote wa michuano hiyo mpaka pale watakapolewa au kumalizika kwa michuano hiyo.

Unaweza kusoma sheria za UEFA hapa: Screen Shot 2014-11-05 at 11.52.20 AM

Swali Je Liverpool wamevunja sheria kwa kuchezesha kikosi dhaifu au Je wataadhibiwa?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here