Home Kitaifa MAXIMO VS PLUIJM – MAONI YA SHABIKI WA YANGA KUHUSU UFUNDISHAJI WA...

MAXIMO VS PLUIJM – MAONI YA SHABIKI WA YANGA KUHUSU UFUNDISHAJI WA MAKOCHA HAWA

1595
0
SHARE

Yanga Chini Ya Pluijm
Timu Ilikuwa Inacheza Mpira Ambao Kila Mtu Alikuwa Anaufurahia,
Wachezaji Waliweza Kucheza “Lateral Passes” Hizi Ni Pass Ambazo Wachezaji Upiga Kutoka Upande Mmoja Kwenda Mwingine, Yaani Kuhamisha Muelekeo Wa Timu Kiuchezaji,
Lakini Pia Waliweza Kucheza “Diagonal Passes” Hizi Zinaitwa Pass Mstari Ambapo Uanzia Kwa Golikipa Kwenda Kwa Beki Zake, Hatimaye Kiungo Cha Chini Kinapokea Mpira Na Kuanza Kuugawa Kwa Viungo Wa Pembeni Au Katikati Kulingana Na Beki Za Wapinzani Zilivyofunguka…Hapa Ndipo Ubora Wa Number Sita Unapoonekana
Timu Ilikuwa Inafunga Magoli Mengi Ambayo Yalikuwa Yanatengenezwa Katika Njia Zake Za Mpira,
Haikushangaza Kuona Mwisho Waa Ligi, Hamisi Kiiza Akiwa Na Idadi Mzuri Ya Magoli, Mrisho Ngasa Naye Akiwa Na Idadi Mzuri Pia Ya Magoli, Kavumbagu Naye Akiwa Na Idadi Mzuri Ya Magoli, Hussen Javu Akionekana Super Sub, Ambaye Aliweza Kutengeneza Na Kufunga Magoli, Leo Hii Timu Inacheza Ikisubiri Fulani Afunge, Eti Tunadanganyana Kuwa Huyu Yupo Kwa Ajili Ya Kufunga Tu, Na Zaidi Tunalazimishana Kuwa Tumpe Muda, Wakati Ata Dalili Za Mchezaji Husika Kubadilika Hazipo

pluijm
Ndiye Kocha Pekee Aliyeweka Record Nchini Tanzania Yakutoa Mfungaji Bora Wa Klabu Bingwa Afrika,Ndani Ya Timu Ambayo Alikuwa Anaifundisha (Mrisho Ngasa)
Haya Yote Aliweza Kuyafanya Kwa Sababu Mfumo Wa Timu Katika Uchezaji Ulikuwa Unaruhusu, Aliwapa Wachezaji Uhuru Wa Kucheza Mpira Uwanjani Na Kufunguka Zaidi, Ndiyo Maana Haikushangaza Ruvu Shooting Ilipopigwa Goli Saba
Cha Ajabu Zaidi Huyu Mzee Hakuwa Na Maneno Mengi, Na Ilikuwa Vigumu Mno Kumsikia Mara Kwa Mara Kwenye Mavyombo Ya Habari
Ushauri Wake Ambao Aliutoa Kwa Uongozi Kuwa Timu Isajili Kiungo Wa Chini Mmoja Na Striker Mmoja Kutoka Timu Ya Chelsea Ya Ghana Nafikiri Ungeweza Kuibeba Yanga Zaidi Katika Msimu Huu Wa Ligi.
Aliishi Miezi Sita Tu Ndani Ya Yanga, Lakini Alionyesha Ubora Na Thamani Ya Taaluma Yake, Mda Mwingine Mambo Kama Haya Ni Kipaji, Na Ni Watu Wachache Wanayaweza, Ndiyo Maana Wala Hakuitaji Mwaka Mzima Kuonyesha Ubora Na Thamani Yake
Aliondoka Akiwa Na Kadi Ya Uanachama Wa Yanga, Lakini Pia Sijawahi Kusikia Mdau Yeyote Akitilia mashaka Uwezo Wake Wa Ufundishaji….
Kipindi Yupo Huyu Mzee Yanga Ilifikia Kiwango Kikubwa Cha Soka, Waliitaji Muendelezo Kidogo Tu Kufikia Kiwango Ambacho Wangeweza Kushindana Na Timu Bora Barani Afrika Na Ushindani Wangeweza Kuonyesha…
Kwa Sasa Baada Ya Yanga Kupiga Hatua Mbele Kiufundi, Imerudi Nyuma Kiufundi, Unasema Unajenga Timu, Utajengaje Timu Wakati Ilishafika Katika Kiwango Bora Cha Uchezaji? Huu Ni Uchizi
Usinizibe Mdomo, Mimi Si Mfuasi Wa Falsafa Ya Soka Ya Maximo Ukiniona Mbaya Kwa Kusema Ukweli, Utajua Mwenyewe, Yanga Inahitaji Kocha Aina Ya Pujjin….Maximo Hana Jipya..

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here