Home Kimataifa LA LIGA; Real Madrid yakwea kileleni kwa mara ya kwanza msimu huu,...

LA LIGA; Real Madrid yakwea kileleni kwa mara ya kwanza msimu huu, Messi akishindwa kuvunja rekodi ya Termo Zarra.

1168
0
SHARE

Matokeo ya kushtusha zaidi katika ligi kuu ya Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita ni yale ya kichapo cha FC Barcelona katika uwanja wa Camp Nou. Celta Vigo ( timu ambayo msimu uliopita ilikuwa chini ya Luis Enlique kocha wa sasa wa Barcelona) ilipata ushindi wa kwanza katika dimba la Camp Nou baada ya miaka 41.

Baada ya kufungwa mabao 3-1 katika ‘ Clasico’ wiki moja iliyopita, Barca ilijikuta ikipoteza kwa mara ya pili msimu huu na kwa mara ya kwanza chini ya Enlique katika uwanja wa nyumbani. Joaquin Larrivey alifunga bao pekee kwa wageni katika dakika ya 55. Lionel Messi alijitahidi kufurukuta na kufunga ili kuifikia rekodi ya mshambulizi wa zamani wa Real Madrid, Terme Zarra kama mfungaji bora wa muda wote wa La Liga. Golikipa Sergio Alvarez alikuwa kikwazo kikubwa kwa washambuliaji wa Barca.

james-rodriguez-gol-real-madrid-vs-granada_rjwgu16wcx1k1ghi1sshh75ge

Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo aliendelea na tabia yake ya kufunga mabao. Ronaldo alifunga bao la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya pili tu ya mchezo katika uwanja wa Estadio Nuevo Los Carmenes. Mfungaji bora wa kombe la dunia, James Rodriguez alifunga mara mbili katika dakika za 31 na 84 huku Karimu Benzema akifunga mara moja katika dakika ya 56 na kuifanya timu yao iondoke ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Granada.

Kwa ushindi huo, Los Blancos wameenda juu ya msimamo. Mabingwa watetezi Atletico Madrid walichomoza na ushindi wa mabao 4-2 katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Cordoba. Mshambulizi, Mfaransa, Griezman alifunga mabao mawili, Mari Mandzukic na Raul Garcia pia walifunga kila mmoja na kuendelea kukinyanyua kikosi cha Diego Semeone ambacho kilianza kwa kusuasua msimu huu.

MATOKEO MENGINE….

REAL SOCIEDAD 0- MALAGA

ATHLETIC BILBAO 1-0 SEVILLE

VILLAREAL 1-3 VALENCIA

LEVANTE 2-1 ALMERIA

ELCHE 2-1 ESPANYON

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here