Home Kitaifa KELVIN FRIDAY: ‘Bado sana kuitoa Azam FC katika mbio za ubingwa.’

KELVIN FRIDAY: ‘Bado sana kuitoa Azam FC katika mbio za ubingwa.’

1200
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole,

Kiungo mshambulizi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam FC, Kelvin Friday amesema ni mapema mno kuwaondoa mabingwa hao katika mbio za ubingwa licha ya kupoteza michezo miwili mfululizo. Mchezaji huyu chipukizi bado anauguza majeraha yake ya misuli ambayo yamemfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja sasa na hivyo kutocheza mchezo wowote hadi sasa.

Screen Shot 2014-11-03 at 12.09.27 PM

Akizungumza na mtandao huu mapema siku ya leo, Kelvin ( mfungaji wa bao muhimu zaidi la Azam msimu uliopita wakati wa mchezo dhidi ya Yanga); “ Naendelea vizuri na majeraha, naweza kurudi uwanjani ndani ya muda mfupi ujao”

Azam ilifungwa kwa mara ya kwanza baada ya mechi 38 katika ligi kuu na timu ya JKT Ruvu wiki moja iliyopita katika uwanja wa Chamanzi Complex, ilisafiri hadi Mkoani Mtwara ambako walikutana na kipigo kingine kutoka kwa Ndanda FC.

“ Ligi ni ngumu, imejaa ushindani lakini bado mapema sana kuiondoa Azam katika malengo yake. Cha muhimu ni kujipanga tu kwa ajili ya mechi zijazo. Tuitatumia mapumziko ya kusimama ligi kwa muda ili kujiweka fiti zaidi. Naamini kuna wachezaji wengine walikuwa na majeraha watarudi katika siku za karibuni na timu itarudi katika ubora wake”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here