Home Kimataifa LUIZ ADRIANO NI SAWA NA MESSI, NI USIKU WA WABRAZIL

LUIZ ADRIANO NI SAWA NA MESSI, NI USIKU WA WABRAZIL

699
0
SHARE

Ushindi mkubwa zaidi siku ya jana ni ule ambao wameupata Shakhtar Donetsk ya Ukraine dhidi ya wenyeji BATE Borisov. Mbrazil, Luis Adriano amekuwa mchezaji wa pili katika michuano ya mabingwa ulaya kufunga mabao matano katika mchezo mmoja. Adriano alifunga mabao matano katika uwanja wa Borisov Arena na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 7-0. Shakhtar walifumga mabao 6-0 hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.

Ulikuwa ni usiku wa Wabrazil, Alex Teixera alifungua kalamu ya mabao katika dakika ya 11, Adriano akafunga bao la pili na la kwanza kwa upande wake kwa mkwaju wa penalti, Mbrazil mwingine, Douglas Costa akafunga bao la tatu kabla ya Adriano kufunga mabao mengine matatu katika dakika za 37, 40 na 44. Mshambulizi huyo alifunga bao lake la tano la mwisho katika dakika ya 82 kwa mkwaju wa panalti na kutengeneza ushindi wa mabao 7-0 kwa timu yake ikicheza ugenini. Mabao yote saba ya Shakhtar yalifungwa na wachezaji raia wa Brazil.

VInara wa kundi hilo la mwisho, FC Porto ilichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao. Kiungo mshambulizi, Ricardo Quaresma aliwafungia wenyeji bao la pili zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo umalizike katika dimba la Dragao Kiungo, Hector Herrera aliwafungia wenyeji bao la kuongoza katika dakika ya 45, lakini bao hilo lilifutwa na mshambulizi kinda, Guillermo Fernandez katika dakika ya 58. Porto inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi saa walifuatiwa kwa karibu na Shakhtar wenye pointi sita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here