Home Kimataifa LIVERPOOL vs REAL MADRID; Mabingwa mara 15, ni Sterling au C.Ronaldo?.

LIVERPOOL vs REAL MADRID; Mabingwa mara 15, ni Sterling au C.Ronaldo?.

1921
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole,

Baada ya mabao 40 kufungwa katika michezo nane ya usiku wa jana katika ligi ya mabingwa ulaya, ‘macho na masikio’ yataelekezwa jijini, Liverpool, England wakati miamba ya ulaya, klabu za Liverpool na Real Madrid zitakapopambana kwa mara ya tatu katika historia ya michuano hiyo. Kumbuka, unapozizungumzia klabu hizo mbili tambua kuwa ‘ unazungumzia mabingwa wa jumla mara 15 wa michuano.

Liverpool imetwaa taji hilo mara tano, mara ya mwisho walitwaa mwaka 2005, Real ni mabingwa mara kumi, huku wakitetea ubingwa huo msimu huu… ‘ Vita ya Jogoo na watoto wa kifalme’, The Reds ndiyo jina la utani la ‘ majogoo wa Merseyside’, ‘ The White’ jina la utani la wakali wa Madrid, timu hizo zinakutana huku kila upande ukiwa na sababu muhimu za kushinda mechi.

Golikipa, Simon Mignolet atasimama lango wakati mshambulizi hatari, Cristiano Ronaldo akitafuta bao la 70 katika michuano hiyo ili kuwa mchezaji wa pili kufikisha idadi ya mabao. Madrid itakosa huduma ya kiungo wake mshambulizi, Gareth Bale na jambo hilo linaweza kuwa nafuu kwa walinzi wa Liverpool. Lovren na Martin Skertel walianza katika safu ya ulinzi wa kati siku ya Jumapili iliyopita ‘ katika ushindi wa maajabu’ dhidi ya QPR katika uwanja wa ugenini. Wawili hao walishuhudia wakiruhusu mabao mawili katika muda wa dakika tatu za mwisho.

Mshambulizi, Jorge Vargas alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 87 na kufuta bao la kujifunga la mlinzi, Richard Dunne dakika 20 nyuma. Kiungo mshambulizi, Phillipe Coutinho alifunga bao la pili kwa timu yake katika dakika ya 90, lakini Vargas akatumia udhaifu wa walinzi wa kati wa Liverpool kusawazisha katika dakika hiyo ya mwisho ya mchezo.

Liverpool ilipata ushindi wa kwanza ikicheza ugenini msimu huu lakini bado wanatakiwa kujizatiti katika idara ya ulinzi na ile ya mashambulizi. Glenn Johnson na Jose Enlique wataanza katika nafasi za ‘ beki 2, na 3’, watakutana na wachezaji wenye kasi kama, C.Ronaldo, Javier Hernandez ambaye kocha, Carlo Ancelotti atamuanzisha sambamba na C.Ronaldo na James Rodriguez.

article-2458816-18794DC200000578-941_634x423

KUMUANZISHA, SAM KHEDIRA, Carlo anaweza kucheza ‘ kamari’ na kumpanga ‘ mchezaji asiyemwani sana’, Khedira katika eneo la kiungo. Licha ya kutopata nafasi katika kikosi cha kwanza, mshindi huyo wa kombe la dunia anaweza kuwa mchezaji muhimu sana kwa Real watakapocheza katika ‘ uwanja wenye kelele sana za nyimbo zenye kuisifu na kuipa moyo timu ya nyumbani’.

Anfield ni uwanja mgumu kwa timu za ulaya, bila shaka, Carlo anaweza kuwa anajua kuhusu hilo lakini atafanyaje ili kupata ushindi?. Ni kocha mwenye mbinu bora, lakini atalazimika kupanga ‘ timu ngumu ‘. Real ni timu kali katika mashambulizi, ila Liverpool ni timu ‘ imara’ katikati ya uwanja. Nahodha, Steven Gerrard ambaye alifunga mara mbili katika ushindi wa mabao 4-0, Machi 10, 2009 ataanza sambamba na ‘ kundi la yosso ‘ katikati ya uwanja.

Joe Allen amepona lakini atakuwa na nafasi ndogo ya kuanza katika kikosi cha kwanza mbele ya Jordan Herndason, Coutinho, Adam Lallana na Rahim Sterling katika nafasi ya kiungo. Luka Modric mchezaji wa zamani wa Tottenham ataanza kama mchezesha timu-mkuu, Ton Kroos na Isco pia walianza katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Levante, Jumamosi iliyopita. Ili kuidhibiti mechi, Carlo anaweza kumuweka nje, Isco na kumchezesha Khedira ambaye alicheza vizuri sambamba na Kroos katika kombe la dunia wakiwa na timu ya taifa ya Ujerumani.

1407869805087_lc_galleryImage_Real_Madrid_team_players_

Wote wawili ( Khedira na Kroos) ni wakabaji wazuri, pia wanashambulia na kufunga mabao. Itakuwa ngumu kumuweka, Hernandez katika benchi kwa kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United anawafahamu Liverpool. Kumchezesha, Isco inaweza kuwa kamari pia kama ambavyo anaweza kufanya hivyo kwa Khedira, lakini katika mechi ambayo, Real itapokea ‘ mashambulizi mengi ya Kiingereza’, mchezaji wa Hispania, Isco hatafaa kwa kuwa si mkabaji.

Kroos hushambulia kwa mipira mirefu, ni kiungo ambaye anaweza kutawanya mipira sehemu nyingi za uwanja kwa pasi zake ndefu-timilifu, hivyo ni bora kumchezesha Khedira ili kwenda sambamba na ‘ viungo wa kisasa’ wa kikosi cha Brendan Rodgers.

2440755_big-lnd

LIVERPOOL NI ‘ BUTU’ lakini mshambulizi, Mario Balotelli anapewa nafasi ya kufanya mambo makubwa katika timu hiyo licha ya uhamisho wake wa kutoka, AC Milan kutozaa mabao hadi sasa. Mario ataanza katika safu ya mashambulizi kama mchezaji huru. Nyuma yake atacheza kijana anayenyumbulika, Sterling na wachezaji hao vijana wanaweza kuwaangusha, Real. Ikel Casillas atasimama langoni licha ya kiwango chake kuwa cha wasiwasi, kama Liverpool watalenga vizuri mipira yao katika goli la Casillas wanaweza kufunga na pengine kushinda mechi.

Ni wachezaji wawili tu wenye utulivu katika safu ya ulinzi ya Real Madrid. Nahodha, Casillas na kinda, Nacho ndiyo huwa hawapaniki ‘ mambo yanapokwenda mrama’, Pepe, Sergio Ramos na Marcelo wote ni wachezaji ‘ wasiotabirika’, hawaogopi kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu, itakuwaje dhidi ya vijana wasumbufu wa Liverpool. Liverpool ilishinda, 1-0 Santiago Bernabeu miaka sita iliyopita, wakashinda 4-0 Anfield katika mchezo wa marejeano, watashinda tena dhidi ya ‘ Real Dozi’

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here