Home Kitaifa HARUNA NIYONZIMA: KIUNGO FUNDI ALIYEANZA KUAGA YANGA

HARUNA NIYONZIMA: KIUNGO FUNDI ALIYEANZA KUAGA YANGA

4953
0
SHARE

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
WAKATI mchezaji bora wa dunia 2008 na 2014, Cristiano Ronaldo anaeleza kuwa mafanikio yake kisoka yametokana na maamuzi magumu ya rafiki yake, kiungo fundi Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ wa Yanga anasema mafanikio yake kisoka yametokana na shemeji yake.
Ronaldo anakiri kuvuma kwake kisoka kumetokana na ‘maamuzi ya Yesu’ ya rafiki yake wa karibu, Albert Fantrau.
“Ninapaswa kumshukuru rafiki yangu Albert kwa kuwezesha uwapo wangu kisoka. Tulicheza pamoja katika klabu moja ya vijana. Watu wa Sporting (Lisbon) walipokuja, walituambia kwamba atakayefunga magoli mengi ndiye alistahili kuchukuliwa kwenda kwenye akademi yao.
Tulishinda mechi ile 3-0, Nilifunga goli la kwanza, Albert alifunga la pili kwa kichwa, na goli la tatu ndiyo lilimshangaza kila mmoja. Albert alikwenda moja kwa moja na kipa. Nilikuwa ninakimbia nyuma yake, alimzunguka kipa, kilichokuwa kimebaki kukifanya ni kuugusa tu mpira uingie kwenye lango lililokuwa tupu.
Lakini, alinipa pasi na nikafunga. Nilikubalika kwenda kwenye akademi. Baada ya mechi, nilimfuata na kumuuliza “Kwa nini” na akanijibu; “Wewe ni mzuri kuzidi mimi”.

Haruna-Niyonzima1
Kwa Niyonzima ni tofauti kidogo. Anasema aliupenda mpira wa miguu kutokana na uwezo uliokuwa ukioneshwa na kaka zake uwanjani lakini shemeji yake aliyemtaja kwa jina moja la Athuman, ndiye aliyempa moyo wa kufanya vizuri zaidi kisoka.
“Kaka zangu walikuwa wachezaji wazuri, nilishawishiwa na makocha wa eneo nilipozawaliwa lakini shemeji yangu ndiye aliyenifanya nilipende zaidi soka. Athuman ndiye mtu wa kwanza kuninunulia viatu vya soka,” anasema Niyonzima.
“Viatu viliniongezea nguvu ya kucheza soka, nikafanya vizuri na kusajiliwa na Etincelles (2005) baadaye Rayon Sports (2006–2007) kisha APR (2007-2011), zote za Rwanda) kabla ya kujiunga na Yanga 2011. Naukumbuka pia mchango wa kocha (Mjerumani Michael) Nees aliyeniita kwa mara ya kwanza timu ya taifa,” anasema zaidi mzaliwa huyo wa Gisenyi, Rwanda.
Tangu 2007 Niyonzima mwenye urefu wa m1.67  ( futi 5.5) ameichezea timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ mechi 60 na sasa ndiye nahodha wa timu hiyo.
yanga
AANZA KUAGA KIANA YANGA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Niyonzima aliuambia mtandao huku kuwa hana uhakika kama ataendelea kuitumikia timu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi), aliweka wazi kuwa hana uhakika wa kuendelea kucheza soka nchini baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Niyonzima (24) anasema mkataba wake na Yanga utamalizika mwishoni mwa msimu huu na hana uhakika kama ataongeza mwingine maana mpaka sasa hajazungumza lolote na uongozi wa Wanajangwani kuhusu hatma yake.
Lakini, kiungo huyo aliyerejea katika makali yake msimu huu akifunga goli moja na kupika moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu baada ya ‘kufulia’ msimu uliopita, aliweka wazi kuwa kamwe hatasitaafu soka pasipo kucheza katika nchi zilizoendelea kisoka.
“Kila mwaka una mambo yake. Nilikumbana na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kuugua, lakini kuna watu hawakuelewa hilo,” anasema Niyonzima ambaye licha ya kusumbuliwa na malaria sugu msimu uliopita, nyumba anayoishi Magomeni Makuti jijini iliungua usiku wa kuamkia Oktoba 3, mwaka jana.
“Ndoto zangu ni kucheza katika nchi zilizoendelea kimpira. Siwezi kumaliza soka langu pasipo kucheza huko,” anasema zaidi kiungo huyo huku akikataa kuweka wazi nchi hizo kwa madai kwamba “muda bado haujafika.”
Niyonzima mwenye urefu wa m1.67  ( futi 5.5), alitua Yanga Juni 23, 2011 akiipa ubingwa wa VPL na Kombe la Kagame klabu hiyo ya Jangwani.
Kabla ya kutua Tanzania, nyota huyo mwenye mtoto mmoja, Ramsi (5), alizichezea klabu za Etincelles (2005), Rayon Sports (2006–2007) na APR (2007-2011), zote za kwao Rwanda.
haruna+niyonzima+kulia+peke+yake+mchukua
MECHI YA WATANI
Kuhusu mechi ya kwanza ya watani wa jadi, Simba na Yanga msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itakayochezwa Jumamosi jijini Dar es Salaam, Niyonzima (24) anasema:
“Itakuwa mechi ngumu na kubwa, kama wachezaji wa Yanga, tunaendelea kujipanga ili tupate ushindi katika mechi hiyo. Tuna kocha mzuri (Mbrazil Marcio Maximo), ninaamini tutafanya vizuri.”
Hata hivyo, kuna taarifa mbaya zimeripoti na baadhi ya mitandao ya michezo nchini leo zikimwonesha mkali huyo akiwa amefungwa bandeji kutokana na kuumia enka mazoezini kwenye kambi yao ya kuiwinda Simba Jumamosi waliyoweka Kunduchi, Dar es Salaam.

KUFULIA 2013/14
Mrwanda huo aliyerejea katika makali yake akiifungia Yanga goli kwa ‘frikiki’ kali baada ya kutoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na beki Kelvin Yondani katika ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu jijini Dar es Salaam Oktoba 5, anasema hakuwa katika kiwango kizuri msimu uliopita kutokana na matatizo mbalimbali.
“Kila mwaka una mambo yake. Nilikumbana na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kuugua, lakini kuna watu hawakuelewa hilo,” anasema Niyonzima ambaye licha ya kusumbuliwa na malaria sugu msimu uliopita, nyumba anayoishi Magomeni Makuti jijini iliungua usiku wa kuamkia Oktoba 3, mwaka jana.

MAFANIKIO NA ANAOWAKUBALI TZ, MAJUU
Anasema anamkubali mchezaji ‘kiraka’ wa Yanga, Mbuyu Twite, raia wa Rwanda mwenye asili ya DRC huku akiweka wazi kwamba kura yake anampa Muargentina Lionel Messi katika vita ya nani mkali inayoendelea kati ya mchezaji bora huyo wa dunia mara nne mfululizo na mchezaji bora wa dunia mara mbili, Mreno Ronaldo.
“Soka limenisaidia kwa mambo mengi katika kuendesha maisha ya familia yangu, sina maisha kama wanayoishi wachezaji wa Ulaya lakini nimefanya mambo makubwa kwetu, ni siri yangu.  Mbinu nyingi za ufundi niliziiba kwa Ronaldo de Lima.
Japo amestaafu soka, mimi bado ninamtambua kama mkali wa dunia na sidhani kama atakuja kutokea mchezaji wa aina yake,” anasema.

MAISHA BINAFSI
Niyonzima, anayependa kula wali/mbogamboga, alizaliwa Februari 5, 1990, ana mke aitwaye Uwineza Naillah na wana mtoto mmoja, Ramsi waliyemzaa Novemba Mosi, 2008. Ni mtoto wa nne kuzaliwa kwenye familia ya watoto 11 (7 me).

ASICHOKISAHAU
Kiungo huyo aliyekuwa katika kiwango cha juu msimu wa 2012/13 ambao Yanga chini ya Mholanzi Ernie Brandts ilitwaa ubingwa licha ya kuanza vibaya ikiwa chini ya Mdenmark Tom Saintfiet, anasema hatayasahau mapokezi ya Wanajangwani wakati akitua nchini Juni 23, 2011 kuitumikia klabu hiyo.
“Ilikuwa siku ya furaha na huzuni. Nilifurahi kwa mapokezi makubwa lakini niliingiwa na huzuni baada ya kuanza kufikiria kama kweli ningeweza kukifanya kile ambacho Yanga walikitaraja kutoka kwangu,” anasema.

ANACHOCHUKIA
Kama ilivyo kwa Warwanda wengi baada ya mauzji ya Kimbali, Niyonzima aliyenyang’anywa namba na Hassan Dilunga katika Kikosi cha Yanga msimu uliopita chini ya kocha Mholanzi Hans van Der Plujim, anasema anachukua uonevu dhidi ya watu wasio na hatia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here