Home Kitaifa NADIR HAROUB, KELVIN YONDAN KUWAVAA SIMBA SC.

NADIR HAROUB, KELVIN YONDAN KUWAVAA SIMBA SC.

602
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole,

Wachezaji wa nafasi ya ulinzi wa kati wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, nahodha, Nadir Haroub na ‘ patna wake katika uchezaji’, Kelvin Yondan wanataraji kucheza katika mchezo wa ‘ Watani wa Jadi’ na mahasimu wa soka la Tanzania, Yanga SC dhidi ya Simba SC katika ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara.

image

Yanga watacheza na Simba katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza msimu huu. Nadir aliumia sehemu ya ‘ paji lake la uso’ wakati akiiwakilisha, Stars katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin mwisho wa wiki iliyopita. Kelvin hakutumika katika mchezo huo kutokana na maumivu ‘ madogo madogo’ ambayo yaliambatana na uchovu wa kucheza mfululizo kwa muda mrefu.

Wawili hao hawakufanya mazoezi siku ya jana na badala yake walikuwa watazamaji tu. Habari za ndani kutoka kwa chanzo chetu cha karibu kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kuwa wachezaji hao ‘ namba 4, na 5’ watacheza siku ya Jumapili. ” Wote wawili ( Nadir na Kelvin) watacheza katika mchezo ujao dhidi ya Simba. Kama mwalimu atawapa nafasi watatumika kwa kuwa majeraha yao ni madogo tofauti na inavyosemwa” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here