Home Kitaifa ZAMUNDA: MUUNDO WA BODI YA LIGI NI KIMEO, TURUDI KATIKA MUUNDO WA...

ZAMUNDA: MUUNDO WA BODI YA LIGI NI KIMEO, TURUDI KATIKA MUUNDO WA KAMPUNI

809
0
SHARE

. CHANGAMOTO KUBWA YA MPIRA WA TANZANIA NI KUJAA VIONGOZI ‘MAGUMASHI’

Rahim Zamunda ni mmiliki wa klabu ya African Lyon iliyo ligi daraja la kwanza Tanzania Bara. Zamunda ni mmoja wa viongozi wa mwanzo kabisa wa klabu za soka nchini kukosoa na kuunga mkono uamuzi wa uundwaji Bodi ya Ligi kama chombo ambacho kitasimamia uendeshaji wa ligi kuu Bara na ile ya daraja la kwanza.
Kufuatia malumbano yaliyopo hivi sasa kuhusu uhalali wa Bodi ya ligi kama chombo huru ambacho kinapinga maagizo ya TFF kudai makato ya 5% kutoka kwa wadhamini kwa klabu za ligi kuu, kiongozi huyo wa Lyon amezungumza kwa kina kuhusu sakata hilo huku akitoa ufafani ni namna gani Bodi ya ligi isivyo huru, huku pia akigusia wakati wa uundwaji wake chini ya rais wa TFF aliyemaliza muda wake, Ndugu Leodgar Chilla Tenga. Ndugu msomaji wa mtandao huu wa www.shaffihdauda.com unaweza kufuatilia mahojiano haya hapa.
Unafuatilia sakata la TFF na Bodi ya ligi, malumbano hayo yanaupeleka wapi mpira wa Tanzania?
“Challenge ya mpira wa Tanzania haiwezi kwenda mbele kwa sababu viongozi wengi ni ‘ magumashi’. Ni watu ambao wanahitaji sifa kuliko chochote kile kutoka katika vyombo vya habari na kukutaa ukweli kuwa soka la Tanzania bila kuwa na viuongozi wenye mipango vu halitapiga hatua”
ZAMU

Je, unafuiatlia kinachoendelekea kati ya Bodi ya Ligi na Shirikisho la soka nchini kuhusu makato ya 5%, ambayo klabu zitakatwa kutokana na mapato yao ya udhamini kutoka kwa Vodacom na AzamTv ambao ni wadhamini wa ligi kuu?
“ Mpira wetu umekuwa kama ‘ muziki wa Taarabu’, watu wanatumia muda mwingi kuzozana kwa mambo yasiyo na umuhimu. Naupenda sana mchezo wa soka na nina sikitika kwa kiasi kikubwa kusikia tatizo ambalo linaendelea kati ya klabu za ligi kuu, Bodi ya Ligi na TFF. Kwa wale wanaojua ukweli ulivyo, timu ya kwanza kuipigia kelele Bodi ya ligi kutoka katika mikono ya TFF ilikuwa ni African Lyon, lakini kuna watu walitokea na kuingilia mipango hiyo ambayo ilikuwa na lengo la kutengeneza chombo huru cha kuendesha ligi. Walifanya uvamizi katika kitu wasicho na ujuzi nacho utaanguka tu na kitakushinda baada ya siku chache, ndicho kinachotokea sasa”
Ilikuwaje wakati ule wa mchakato, mkipigania kutoka katika mikono ya TFF na kuwa chombo huru, kipi kilifanyika na nini matokeo yake?
“ Wakati chini ya uongozi wa Ndg, Leodgar Tenga lengo kuu ilikuwa ilikuwa ni kuwa na kampuni huru ya ligi. Dunia nzima ndivyo inavyofanyika, mafono kuna ncho za Kenya, Uganda, Afrika Kusini zipo katika utaratibu huo, ila kilichotokea ni kwamba, lengo la kuanzishwa Kamati ya Ligi ambayo ilifanya kazi kama inavyofanya hivi sasa Bodi ya ligi. Mimi nilifukuzwa katika uchaguzi wa Bodi ya Ligi kwa sababu nilikuwa nikiuliza baadhi ya mambo yenye umuhimu na tija”

Hali ilikuwaje, je, unafikiri Tanzania ina viongozi bora wa soka?
“ Kuanzia kwenye vilabu hadi ngazi ya juu, viongozi wetu wa mpira ni watu wenye upeo mdogo sana wa uongozi wa mambo ya soka. Hatuna ‘ wati hasa wa mpira’ na kama wapo hawapewi nafasi. TUrudi katika hili la Bodi ya ligi. Bodi ilikuwa na kanuni zake, na kanuni za ligi ambazo klabu zilikubaliana ni kwamba, kila msimu unaookuwa umemalizika, klabu sita za juu ‘ Top Six’ ndizo zitaingia moja kwa moja katika Bodi ya ligi. Mwenyekiti au makamu wake timu yake itakuwa nje ya nafasi sita za juu atakuwa amepoteza nafasi yake katika Bodi ya Ligi. Vilevile kabla ya msimu mpya kuanza, klabu zinatakiwa kukutana katika mkutano mkuu ambao utajadili namna ligi ilivyomalizika na faida/hasara zilizopatikana, lakini ligi imekwisha na hilo halijafanyika, timu hazijakutana kujadili mambo muhimu yaliyotokea msimu uliopita”

ZA

“ Viongozi waliopo hawawezi kazi walizonazo, mara nyingi huwa tunawaita wataalamu wan je kwa ajili ya kutupa kile walichonacho lakini viongozi wetu huwa wanakimbia. Leo hii klabu zinakaa chini na kuanza kupigiana kelele na TFF kwa makato ya asilimia tano! Inashangaza, kwa sababu klabu za ligi kuu zinapata milioni 110 kutoka kwa AzamTV, Milioni 60 kutoka kwa Vodacom ukichanganya na michezo minne wanayocheza na Simba na Yanga kuna zaidi ya milioni 200. Kama klabu zinauwezo wa kuzalisha miradi mingine Na hiyo asilimia tano ikabaki katika maendeleo ya mpira. Kama hizo 5% zitaenda na zitaliwa hapo klabu zinaweza kuhoji zilipo fedha hizo, badala yake watu wanakimbilia kupiga kelele badala ya kwenda kwenye mkutano kwanza.

Kanuni zipoje kwa uwakili wa timu za daraja la kwanza?
“ Daraja la kwanza tuna timu ikishuka daraja itapoteza uwakilishi katika bodi ya ligi. Pamba FC imeshuka daraja kwa maana hiyo daraja la kwanza hatua wawakilishi.. Tuachane na Bodi ya ligi na tuwe na kampuni hivyo ndivyo wanavyofanya nchi nyingine huwa hawana Bodi ya ligi”
Timu gani ambazo zitakiwa kuunda Bodi ya ligi hivi sasa?
“ Azam FC, Yanga SC, Mbeya City, Simba SC, Kagera Sugar na Ruvu Shooting lakini sivyo ilivyo Bodi ya ligi inaundwa na timu gani? Ni zile za msimu uliopita. Vilabu vyenyewe havijijui kwa sababu viongozi wao hawafai licha ya wao kusema wanafaa”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here