Home Kitaifa BIN SLUM: NIPO TAYARI KWENDA MAHAKAMANI, COASTAL WAMEKURUPUKA….

BIN SLUM: NIPO TAYARI KWENDA MAHAKAMANI, COASTAL WAMEKURUPUKA….

702
0
SHARE

Wiki hii klabu bingwa ya zamani ya Tanzania Bara, Coastal Union ilitoa taarifa ambayo inasema kuwa wataipeleka mahakamani Kampuni ya Bin Slum Tyres kwa madai kuwa kampuni hiyo imeendelea kutengeneza ‘ t-shirt’ zenye nembo ya ‘ Sound’ na kuwapa bure mashabiki wa timu hiyo kwenye mechi mbalimbali msimu huu. Coastal imefikia uamuzi huo kwa madai kuwa ni kinyume na utaratibu ambao unakubalika kisheria, kwa kuwa tayari timu hiyo ya Tanga imekwishapata mdhamini mwingine tofauti na Bin Slum.
Bin Slum alikuwa mfadhili/mdhamini wa timu hiyo tangu mwaka 2010 wakati ikiwa ligi daraja la kwanza, alijiweka kando na kuamua kusitisha udhamini wake kwa timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu msimu uliopita, na baadae Ahmed Aurora aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema kuwa, Coastal haikuwahi kunufaika na uwepo wa Kampuni ya Bin Slum, jambo ambalo lilipingwa na Nassor Bin Slum .
Malumbano hayo yalififia kabla ya sasa kuibuka upya, huku safari hii, Coastal wakienda mbali zaidi na kusema kuwa mfadhili huyo wa timu za Ndanda FC ya Mtwara na Stand United ya Shinyanga amekuwa akiendelea kutengeneza ‘T-shirt ambazo zinaonyesha moja kwa moja ni miongoni mwa wafadhili wa timu hiyo.
BIN

“ Nachoweza kusema ni kwamba, Coastal wanaendeshwa na hisia” anasema, Bin Slum na kuongeza; “ Wanachotakiwa kufanya ni kujichunguza wao wenyewe na kutafakari kama kweli wapo na mashabiki wao au wametengana. Ninavyojua mimi mnapokuwa katika hali ya kutoelewana ( mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe), mathalani iki kinachoendelea ndani ya Coastal, mgogoro wao wa kuvuana uanachama walitakiwa kuutatua bila kunihusisha mimi kwa sababu tayari niliamua kukaa mbali na timu hiyo kutokana na yale yalitokea siku za nyuma”
Bin Slum anadaiwa kutengeneza T-shirt hizo huku akiwavalisha na kuwalipia viingilio mashabiki wanaodaiwa wa timu hiyo licha ya mkataba wake na timu hiyo kumalizika. Kiwanda cha kutengeneza Ngano kilichopo mkoani humo ‘ Sembe Flours Mills’ ndiyo wadhamini wa sasa wa timu hiyo;
“ Wasinihusishe mimi katika matatizo yao, wakae na kujiuliza ni wapi wanapokosea na si kujaribu ‘ kunichokonoa’ ili niseme. Nisingependa kuhusishwa katika matatizo yao na mashabiki wao. Ni jambo ambalo linanisikitisha sana na ninazungumza kwa hisia kuwa ili suala wanapolipeleka yatajulikana mengi na mimi nipo tayari kwenda huko wanakotaka ( mahakamani), huko itajulikana zaidi kwa nini mimi niliachana na Coastal Union”
“ Wakati ule nilisema kuwa Coastal Union imekosa viongozi, sasa huu ni wakati ambao Mungu anasaidia mambo hayo kuwa wazi zaidi. Unampelekaje mahakamani mdhamini aliyepita ‘ eti, kwa sababu mashabiki wanavaa jezi zake. Je, itakuwa hivyo kwa mdhamini wa sasa ‘ Sembe’ kama mwakani atakuwa amemaliza mkataba na timu hiyo? Je, naye atapelekwa mahakamani ikiwa mashabiki watavaa jezi zenye kutangaza biashara yake? Mfano mwakani Tanga Cemect wakawa wadhamini je mashabiki watakao vaa sembe watakamatwa na kufunguliwa mashtaka?”
SOUND

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here