Home Kitaifa EXCLUSIVE: SAKATA LA MAKATO YA ASILIMIA 5 – DAMAS NDUMBARO KUPELEKWA KAMATI...

EXCLUSIVE: SAKATA LA MAKATO YA ASILIMIA 5 – DAMAS NDUMBARO KUPELEKWA KAMATI YA NIDHAMU

705
0
SHARE

Sakata la vilabu 14 vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Bara kupitia kwa mwanasheria wao, Dk Damas Ndumbaro, kupingana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kukatwa asilimia tano ya fedha za wadhamini wa ligi hiyo na kutishia kutoshiriki ligi na zitapiga kura ya maoni ya kutokuwa na imani na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ikiwa TFF itatekeleza azma yake, limechukua sura.

Mapema wiki iliyopita, Malinzi aliagiza timu hizo kukatwa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Soka (FDF) ambapo klabu husika zikiwemo Simba na Yanga zimepinga hatua hiyo na kutishia kutocheza ligi kuu kama agizo hilo litatekelezwa na Bodi ya Ligi.

Sasa kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika inaelezwa kwamba Shirikisho la soka nchini limefikia hatua ya kumpeleka mwanasheria huyo Damas Ndumbaro kwenye Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo kutokana na kitendo chake alichokifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here