Home Kitaifa SIFA UTD YA MANZESE YAIFUNGA MILAMBO YA MBURAHATI MABAO 2-1,

SIFA UTD YA MANZESE YAIFUNGA MILAMBO YA MBURAHATI MABAO 2-1,

1226
0
SHARE

Mashindano ya Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup yameendelea jana kama kawaida kwa michezo mitatu kupigwa, ambapo michezo hiyo ni mchezo wa Sifa United dhidi ya Forte Eagle katika Uwanja wa mwalimu Nyerere uliomalizika kwa Sifa kushinda mabao mawili kwa moja.
Mabao yote mawili ya Sifa Utd yalifungwa na mshambuliaji Mhilu ‘Arteta’ wakati lile la kufutia machozi la Fort Eagles almaarufu kama Milambo ya Mburahati liliwekwa kimiani na Hamis Dengwa.
Segerea FC walikuwa nyumbani katika Uwanja wa Benjamini Willium Mkapa maeneo ya Karume Jijini Dar-es-salaam, kucheza na Temeke Squard mchezo ambao ulimalizika kwa timu hizo kufungana mabao mawili kwa mawili.
Mchezo wa tatu hiyo jana ulizikutanisha timu za Makumba FC dhidi ya Same katika Uwanja wa Airwing huko Ukonga, na mpaka muamuzi wa mchezo huo anapuliza kipyenga cha kuashiria mchezo huo kumalizika Makumba FC imeshinda bao moja kwa bila.
Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup itandelea jioni ya leo kwa michezo minne kupigwa, ambapo Boom watacheza na Tabata FC katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Micovila watakuwa na kazi dhidi ya Kijichi Stars Kinesi, Sifa Politan watacheza na Vijana Ilala- airwing wakati Tuamoyo watavaana na Beira Hotspurs Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere.
Michuano hii imezidi kunoga kadri siku zinavyokwenda mbele, kiasi cha kuwavuta hadi wadau mbalimbali wa michezo Nchini kufika katika viwanja tofauti kushuhudia michuano hiyo, miongoni mwa wadau hao ni mchezaji wa zamani wa Simba Thomas Kipese.
20141001_170621(0)
Mshambuliaji wa Sifa Utd Mhilu Arteta akijaribu kuutuliza mpira…….

 

 

20141001_170628

 

20141001_175036Mabeki wa Milambo wakiweka ukuta kuzuia faulo inayopigwa kuelekea langoni mwao……kijiji

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here