Home Dauda TV WAZEE WA MIKEKA: UTABIRI WA KAIJAGE v SUSO LIGI KUU ENGLAND

WAZEE WA MIKEKA: UTABIRI WA KAIJAGE v SUSO LIGI KUU ENGLAND

2524
0
SHARE

KAIJAGE VS SUSO PREMIER LEAGUE PREDICTION

Arsenal V s Manchester city

Kwa mara nyingine arsenal inakumbana na kigogo wa ligi katika mechi ya mapema kabisa.Arsenal itakua ikiingia katika mchezo huo ikikumbuka vipigo vya 6-3 kutoka kwa city,5-0 kutoka kwa Liverpool na 6-0 kutoka kwa Chelsea walivyokumbana navyo ligi ya msimu uliopita wakicheza muda kama wanaocheza leo.Mechi ya leo itakua kipimo sahihi kwa washambuliaji wapya Dany welbeck na Alexis sanchez.Arsene wenger inabidi atumia wachezaji wenye kasi kuipenya ngome ya city kupitia pembeni,itakua ngumu kwa arsenal kupitisha mashambulizi yao kupitia kati kati ya uwanja ambapo ndipo kuna siri ya ushindi ya Manchester city.City hawatakubali kufungwa mechi mbili mfululizo wataendelea kumtumia mchezaji wao mgumu Fernando kuwazuia viungo wa arsenal na kuwapa uhuru Yaya toure,Nasri na Silva kupika mabao kwa washambuliaji wao hatari Dzeko na Aguero wanaotarajiwa kuanza leo.

Kaijage Arsenal 1-2 Manchester city

SUSO Arsenal 1-2 Manchester

Chelsea Vs Swansea Hapa tutashuhudia moja ya timu kupoteza point au timu zote kupoteza point kwa mara ya kwanza katika msimu mpya wa ligi ya uingereza.Chelsea itaingia uwanjani leo kusaka ushindi wan ne mfululizo kama ilvyo Swansea.Mechi itakua ngumu kwa Swansea si kwasababu tu ya timu wanayokutana nayo bali hata uwanja wanaopendakuchezea mechi.Chelsea itaendelea kumtegemea kiungo wao maridadi cesc fabregas ambaye ndie ‘archtect’(msanifu) wa mashambulizi ya Chelsea.Kocha monk atajaribu kufanya kiti kama kile atakachokifanya kwenye uwanja wa old traford kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi.Monk ataendelea kumtumia kiungo mshambuliaji Sigurdsson aliye kwenye kiwango bora kwa kupika magoli matatu na kufunga goli moja mpaka sasa.

Kaijage Chelsea 2 Vs 0 Swansea SUSO

Chelsea 2 Vs 0 Swansea

Palace Vs Burnley Ukiniuliza timu nnazaofikiri zitashuka daraja msimu huu sitaacha kuzitaja hizi timu mbili.Kila moja ina point moja mpaka sasa.Moja inakamata nafasi ya 20 na nyingine imeshika mkia.Steve parish anajaribu kutuaminisha neil Warnock ana ubora ule ule wa pulis.Palace licha ya kumrudisha Wilfred zaha na kuwasajili nyota kama campel na hangeland lakini bado wataendelea kuhaha ili kupata nafasi ya kubaki ligi kuu.Kwa upande wa sean dyche inaonekana amekosa wachezaji wwazoefu wa ligi kuiongoza timu yake.Sean dyche amempa mzigo mzito nyota chipukizi wa timu ya taifa ya vijana ya England dany ings ambao hawezi kuubeba peke yake.

Kaijage palace 2-1 Burnley

SUSO palace 1-0 Burnley

West brom Vs Everton Ukiacha palace na burnley kocha Alan Irvin nae ana nafasi kubwa ya kuitumbukiza west brom shimoni kuliko nafasi ya kubaki ligi kuu.West brom na hull city ndio timu zilizosajili wachezaji wengi msimu huu kila moja ikisajili wachezaji 11.Lakini wachezaji hao akiwemo mshambuliaji raia wa Nigeria aliyevunja rekodi ya usajili wa west brom brown ideye wamekuwa hawana msaada mkubwa kaqtika timu hiyo.Everton wataendellea kufurahia uwepo wa beki zao za pembeni bora kabisa kwenye ligi ya uingereza coleman na baines.Coleman na baines ndio silaha ya ushindindi wa everton kila mmoja akifanya kazi tatu ya kushambulia,kuzuia na kutengeneza magoli.Ukitaka kuizuia everton inabidi uanze kwa kuwazuia coleman na baines.Licha ya everton kuwa na rekodi mbaya kwenye mechi za ugenini lakini sioni wakiangusha point kwenye mechi hii

Kaijage West brom 1 Vs 2 Everton SUSO

West brom 0 Vs 2 Everton

Southampton vs Newcastle

Wakiwa hawajapata ladha ya ushindi nyumbani kwa Southampton katika Mara mbili zilizopita Newcastle wanaenda tena katika uwanja huo wakiwa muda huu hawajapata ushindi wa aina yoyote. Nadhani hii inaendelea kuwa presha kubwa kwa kocha wa Alan Pardew kutokana na aina ya usajiri aloifanya na aina ya matokeo anayopata. Upande wa pili Ronald Koeman anaendelea kupata muunganiko wa wachezaji wake wapya bahati yake kubwa ikiwa ni hana majeruhi katika kikosi alichoanza nacho msimu mpya. Wakati Newcastle wakipata mashaka kwa baadhi ya wachezaji wake kama De Jong, Roland Aarons ambao wote wanaelekea kukosa mchezo huu baada ya kuumia katika timu ya taifa. Itakuwa ni mechi yenye presha sana haswa kwa Newcastle wakiwa wanatamani kupata ushindi lakini muda huu ikiwa katika uwanja mgumu. Nafikirii usajiri bora alioufanya Ronald Koeman mpaka sasa ni kumbakisha Morgan Scherneidarlin.

SUSO SOTON 2 NEWCASTLE 1

Kaijage SOTON 2 NEWCASTLE 1

Manchester united vs Queens Park Rangers

Penginr hii ndio mechi ambayo mashabiki, wachezaji na wapenzi wa Manchester united wataingia wakiwa na imani nayo zaidi. Falcao, Di Maria, Rooney, Mata, Robin Van Persie, Herrera, Rojo, Blind wote wapo tayari kwa mchezo huu. Huu ndo mchezo ambao Van Gaal anatakiwa atuaminishe kwamba yupo katika Mlengo sahihi baada ya kuondoka Welbeck. Ukubwa huu wa kikosi ndio unaotoa nafasi kwa wachambuzi wengi kuendelea kuwa na matumaini juu ya Van Gaal. Lakini hii ni shinikizo kubwa sana kwake, ataingia katika mechi hii akiwa na macho ya watu mgongoni mwake. Tatizo kubwa amabalo watu wengi hawalifikirii sana ni uwepo wa wachezaji wengi wageni katika kikosi cha Manchester na ugeni wao katika ligi, ugumu na nguvu zinazotumika katika ligi ya Uingereza bado zinawapa changamoto ya kutoa kile walichonacho kwa kiwango kikubwa. Na pia bado Egemeo la United lipo katika khali ambayo sio iliyotegemewa naamaanisha Kiungo wa Ulinzi na Beki wa Kati mwenye uzoefu. Kwa upande wa QPR baada ya Harry Redknap kupata ushindi katika mechi iliyopita nadhani atakuwa amepata wazungu wanaita ‘boost’ ama chagizo kuelekea mechi hii. Tatizo kubwa kwao ni ulinzi wao, na ukitizama safu ya ushambuliaji ya United itakuwa kazi kwao. Pengine Van Gaal ameamua kukaba kwa kushambulia yaani njia yake ya kukuzuia wewe iwe kukushambulia lakini napata shaka kidogo,.

SUSO MAN U 2 QPR 0

Kaijage MAN U 3 QPR 0

Liverpool vs Aston Villa

Kama unapenda kufahamu mechi ambazo umpa shida na tabu kubwa Liverpool basi ni mechi dhidi ya Stoke City na pia dhidi ya Aston Villa. Paul Lambert anajua kucheza na Brendan Rodgers. Pamoja na hayo Liverpool inaonekana timu yenye muunganiko mzuri sana haswa kwa wachezaji wageni wanaonekana kuingia vyema katika mfumo wa timu. Hapana shaka wachezaji wao muhimu zaidi kwa sasa ni Raheem Sterling, Sturridge na Jordan Henderson. Hawa ndio askari wa namna Liverpool inavyocheza. Huku Henderson akiwa yule hasiyesemwa sana ndio mchezaji anayefanya kazi nyingi kwa wakati mmoja Liverpool. Fabian Delph ndio nenda kamtizame mchezaji huyu, anajua nini Aston Villa wanataka. Tofauti kubwa ya vikosi hivi mpaka sasa ni mechi walizopitia, huwezi kuwadharau Aston Villa lakini nadhani hii ndio changamoto Yao ya kwanza katika msimu huu. Wanakutana na moja ya timu inayopenda kufunga huku na wao wakiwa na aina ya ulinzi inayoonekana kuwa Imara. Brendan Rodgers anakabiliwa na majeruhi lukuki baada ya Johnson, Skrtel na Flannagan sasa wameongezeka Can na Sturridge pengine na Allen. Hii inaweza kuwa mechi itakayoshuhudia akipanga kikosi chenye muono wa ushambuliaji zaidi baada ya viungo wake wakabaji wengi kuumia. Itakuwa mechi itakayoamuliwa na mbinu za makocha zaidi. SUSO LIVERPOOL 3 VILLA 1

Kaijage LIVERPOOL 2 VILLA 1

Sunderland vs Tottenham

Stadium of light. Itakuwa ni mchezo ambao wanakutana wanyama waliojeruhiwa wanaotamani kupata furaha. Gus Poyet anaonekana ni mwenye kusuka kikosi chenye nidhamu sana kwa wachezaji kufuata majukumu waliyopewa. Upande wa pili wanakutana na kocha aliye na mbinu na mwenye kupenda soka ka kuvutia. Nadhani hiki ndicho kilichomponza Mauricio Pochettinho katika mchezo uliopita dhidi ya Liverpool. Hili ni jambo ambalo Pochetinho inabidi alitizame maana Gus anapenda kucheza na nafasi. Nadhani itakuwa ni mechi utakayoamriwa kuwa tofauti ndogo sana ya magoli na nadhani Totenham wana nafasi zaidi. Shinikizo kubwa kwa Sunderland ni kukosa kwao ushindi katika mechi walizocheza japo wamepoteza mechi moja Tu na sasa wana point 2. Bado hawajapta ile kasi waliomaliza nayo ila ni timu ambayo inaonekana inaweza kufunga lakini pia haikuzuii wewe kuwafunga.

SUSO: S’LAND 0 TOT 1

Kaijage S’LAND 1 TOT 1

Stoke City Vs Leicester

Ushindi dhidi ya Manchester city ugenini? Ndio hili linaweza kuwa chagizo kubwa sana kwa kikosi cha Stoke City. Lakini pamoja na hayo moja ya timu zilizopata kuwa na ratiba ngumu ya Mwanzo basi ni Leicester. Katika mechi tatu za mwanzo wamecheza dhidi ya Everton, Chelsea Kisha Arsenal kwa timu iliyopanda daraja huu ulikuwa mtihani mkubwa sana na kupata japo point mbili katika michezo hiyo ni jambo linaloweza kukuashiria kuwa wana kitu cha kutupa msimu huu. Ujio wa mkongwe Esteban Cambiasso unaweza kuwa chachu ya namna ya wao kucheza pia wamesajiri wachezaji wengi wenye uzoefu katika ligi, Albrighton na wenzake. Nadhani Leicester ni moja ya timu zinazopaswa kutizamwa kwa jicho la tatu kwa yeyote anayekutana nao. Wanacheza kwa kuelewana na hawana hofu ya kushambulia. Wana timu zaidi ya staa katika timu. Ni moja ya timu zinazocheza kwa nidhamu na mbinu. Upande wa stoke wanarejea katika uwanja wanaopenda kupatia matokeo zaidi. Britannia stadium sio sehemu nyepesi hata kidogo kwa wapinzani. Tatizo kubwa la Stoke inaweza kuwa Miram Diouf kama akiwa fiti kutoka katika mechi za kimataifa

SUSO STOKE 1 LEICESTER 1

Kaijage STOKE 1 LEICESTER 0

Hull city Vs West ham Kama nilivyosema awali hull city ni miongoni mwa timu zilizosajili wachezaji wengi pamoja na west brom, ila Hull city wamesajili ‘quality players’ ukifananisha na west brom.Mshambuliaji raia wa Uruguay aliyeamua kuitosa benfica Abel Hernandez,Mohamed diame,Gaston Ramirez,Ben arfa,Thom ince,Michael Dawson.Hapa kwa haraka utagundua makamu bingwa hawa wa fa cup kuna kitu wanakitafuta msimu huu.Nafikiria ukuta wa Davies na Dawson,huku nikiwaza kiungo cha Mohamed diame na Huddlestone na Livermore bila kusahau safu ya ushambuliaji itakayoongozwa na Hernandez,Snodgrass na Ince utaona kuwa chui wa bruce watasumbua sana msimu huu.west hama waliyomuuza diame upande wa pili watakua na kazi ngumu kupata ushindi kwenye uwanja wa KC stadium licha ya kuwa na nyota kama Mauro zarrate na alex song

Kaijage Hull city 2- 1 Westham SUSO

Hull city 1- 0 Westham

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here