Home Utabiri wa Mikeka UTABIRI WA MIKEKA JUMA HILI…

UTABIRI WA MIKEKA JUMA HILI…

2428
0
SHARE

KAIJAGE Vs SUSO NDANI YA LIGI KUU UINGEREZA
BURNLEY Vs MANCHESTER UNITED
Kwa mara nyingine uwanja wa turf moore utakalibisha jabali lingine la soka ,Manchester united.Burnley na Manchester united zitakuwa zinaingia kwenye mchezo huo huku zikiwa hazijaonja ladha ya ushindi kwenye msimu huu mpya wa ligi ya uingereza.Manager sean dyche ataendelea kumtumainia mshambuliaji wake hatari Danny ings kumpatia ushindi wa kwanza huku Louis va gaal wa Manchester united mwenye msukumo mkubwa wa kupata matokeo chanya anatarajiwa kumtumia kwa mara ya kwanza mchezaji ghali zaidi kusajiliwa katika ligi kuu ya England Angel dimaria.Di maria anatarajiwa na washabiki wengi Duniani kuleta chachu ya ushindi kwenye timu ya Manchester united.
Kaijage Burnley 1-2 Manchester united
Suso Burnley 1-2 Manchester united

MANCHESTER CITY Vs STOKE CITY
Stoke city inatarajiwa kumkaslibisha kwa mara ya kwanza mshambuliaji wao mpya waliomsajili kwa mkopo kutoka Chelsea Victor moses.Kocha Manuel Pellegrini akitarajiwa kuendelea kuwatumia washambuliaji Edin Dzeko na Jovetic huku mshambuliaji kipenzi wa Manchester city Sergio Aguero akiendelea kutumika kama mchezaji wa hakiba mpaka pale atapokuwa fit.Utakuwa mtihani mgumu kwa kocha wa zamani wa Manchester city mark hughes kusaka ushindi wa kwanza wa ligi kwenye uwanja mgumu wa etihad.
Kaijage Manchester city 3-0 Stoke city
Suso Manchester city 2-0 Stoke city

NEWCASTLE Vs PALACE
Mshambuliaji Wilfred Zaha kwa mara nyingine tena anarejea kwenye timu yake ya zamani ya Crystal palace kwa mkopo wa muda mrefu.Licha ya Wilfred Zaha palace wamemrudisha pia kocha wao wa zamani Neil Warnock kuziba nafasi iliyoachwa na kocha pulis.Newcastle itamkosa kiungo wao tegemeo Cheick tiote na beki yanga mbiwa,Lakini jack colback anatarajiwa kuvaa vyema viatu vya Cheick tiote kipindi hiki anchoauguza majeraha.Newcastle wataingia kwenye mechi na palace huku wakiwa na historia nzuri dhidi ya palace kwa mechi zilizopita,kwenye mechi nane zilizopita wameshinda mechi 7 na kutoa sare mechi 1
Kaijage Newcastle 2-0 Palace
Suso Newcastle 2-0 Palace

QPR Vs SUNDERLAND
Mshambuliaji mpya wa QPR Eduardo vargas ataendelea kusubiri kibali ili aweze kuvaa uzi wa blue na mweupe.QPR mpaka sasa haijapata hata point moja kwenye ligi kuu uingereza itakuwa na kibarua kigumu kuwazuia vijana wa gus poyet kupata matokeo. QPR imepata pigo baada ya kiungo wao alejandro faurlin kuumia na kukosa michezo yote iliyobaki ya ligi kuu uingereza.Kiungo jack rodwell anatarajia kuendelea kutakata huku gus poyet akiumiza kichwa kutokana na kuwa na safu ya washambuliaji butu inayoongozwa na altildore na fletcher.
Kaijage QPR 0-0 Sunderland
Suso QPR 1-1 Sunderland
SWANSEA Vs WBA
Kocha garry monk anatarajiwa kuendelea na mfululizo wa ushindi watapoikabili WBA.Garry monk ataingia kuikabili WBA akikumbuka ushindi wa mechi mbili zilizopita haswa ule alioupata kwenye uwanja wa old traford kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi.Washambuliaji hatari Bonny na Gomiz wanatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji ya Swansea huku wakisaidiwa kwa karibu na kiungo mshambuliaji Sigurdson.Mgiriki Georgios Samaras wa WBA ataendelea kusubiri mechi yake ya kwanza mpaka pale atapokuwa fit.Kocha Alan Irvine ataendelea kuwatumia washambuliaji wake victor anichebeBerahino,Sessegnol na mshambuliaji aliyevunja rekodi ya usajili wa WBA Ideye kusaka matokeo chanya kwenye uwanja wa liberty.
Kaijage Swansea 1-1 WBA
Suso Swansea 1-1 WBA

Everton Vs Chelsea

Mechi ngumu na nzuri kutizama. Ni kipimo na jaribio la kwanza kwa Mourinho na kikosi kama ilivyokuwa kipimo kwa Arsenal. Silaha kubwa ya Everton ni kufunga kwa sasa, ingawa na wao wanaonekana kukubali kuruhusu magoli pia. Itakuwa mechi yenye Kasi haswa upande wa Everton wanaopenda kutumia upande wa pembeni haswa silaha Yao ikiwa mabeki wa pembeni walio na kasi,unatakiwa uwatizame hawa wanavyoshambulia kuliko wanavyokaba. Bado Everton wanatakiwa wabadilike katika ulinzi, Cesc Fabregas, huyu ndio wa kumtizama kwa sasa, anaijua ligi na maamuzi yake kwa sasa ndio yanaweza kuwa na matokeo sana kwa upande wa Chelsea kwa sasa Acha tusubiri kuona kama vazi jipya hili la Mourinho ni je linampendeza au arudi katika park the bus.
Suso: Everton 1 Chelsea 2
Kaijage Everton 1 Chelsea 1

Tottenham vs Liverpool

Mauricio Pochetino vs Brendan Rodgers
Uzuri wa kwanza wa hii mechi ni falsafa za hawa makocha wawili hawana tofauti sana, wote wanataka timu icheze mpira mzuri na ifunge. Pengine Liverpool ndio itakaribisha dimbani nyota wake wote iliowasajili msimu huu. Ingawa jicho na sikio la mpenzi yoyote wa Liverpool likiwa kwa atakachofanya Mario Balloteli maana huyu ndie atakaeweka matumaini ya mashabiki hai au kuyazorotesha lakini bado nadhani silaha Yao itategemeana kuelewana kwao na ninaona Markovic akiwa na siku nzuri kama akicheza. Totenham wameanza msimu vyema sana na Mauricio inaonakena anakipatia kikosi kuanzia namna ya uchezaji mpaka matumizi ya wachezaji wenyewe sidhani kama itakuwa mechi rahisi hasa kwa Liverpool.
Utabiri:
Suso Tot 1 Liverpool 1
kaijage Tot 1 Liverpool 2

Leicester Vs Arsenal

Bado itaendelea kuwa ratiba ngumu sana kwa hii timu iliyopanda daraja, ni ratiba itakayokuwa ya kuwachosha kwa kipindi hiki. Arsenal wanatoka kupata ushindi katika mchuzo wa ligi ya mabingwa, Aaron Ramsey ambaye kwangu namuona kama Lampard mpya katika kufunga anarejea, hii itakuwa mechi nzuri sana ukizingatia aina ya uchezaji ya Leicester wakiwa nyumbani. Alexis Sanchez, amekuwa kimya kiasi lakini ndio wakati wake wa kuonyesha thamani yake huku Mesut Ozil akitakiwa kurejesha makali yake. Vinginevyo Arsenal inabidi washindane na kasi ya Leicester wakiwa na mpira na presha ya ule uwanja, nawaona wakiruhusu goli.
Utabiri:

Suso: Leicester 1 Arsenal 2
kaijage Leicester 0 Arsenal 2

West ham Vs Southampton

Southampton bado hawajapata ushindi katika ligi. Bado wanatafuta muunganiko hasa katika safu ya ushambuliaji kutokana na kuondokewa na watu wao muhimu pale mbele huku Jay Rodriquez akiendelea kuwa majeruhi. Huu ni muda ambao Hapana shaka Ronald Koeman ataendelea kuwa na presha ya kutuaminisha kuwa kafanya usajiri sahihi na kuwa safu ya ushambuliaji yake ni nzuri. Tatizo walilonalo West ham ni wingi wa majeruhi ambao Wako pia wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza. Silaha ya Sam Allardayce ya kwanza itakuwa uwanja wa nyumbani. Kwa haraka mechi inaonekana kama suluhu lakini nadhani Southampton ana kitu cha kupata katika mechi hii na pengine ushindi katika kombe la ligi utawapa motisha zaidi.

Suso: West ham 1 Southampton 2
kaijage West ham 1 Southampton 1

Aston Villa vs Hull City
Kwa upande wa Aston Villa nadhani kurejea kwa goli kipa wao Brad Guzan katika milingoti na beki Vlaar kutawapa khali ya kujiamini zaidi na kucheza vyema zaidi. Wakiwa nyumbani nadhani mechi ambayo Fabian Delph inabidi aitendee haki thamani ya kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza. Naamini huyu Ndo mwenye matokeo kwa kiasi Fulani ya Asto Villa. Hull city watawategemea watu wao walewale na kurejesha kikosini akina Huddlestone na Ince. Itakuwa ni mecho ngumu yenye kuhitaji matokeo.
Suso: Astonvilla 1 Hull city 0
Kaijage Astonvilla 2 Hull city 1

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here