Home Kitaifa  SOMA UCHAMBUZI WA AZAM FC v EL MERREIKH, ROBO FAINALI KOMBE LA...

 SOMA UCHAMBUZI WA AZAM FC v EL MERREIKH, ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME

1162
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kagame Cup, Azam FC watakuwa uwanjani jioni ya leo kuwakabili timu ya El Merreikh ya Sudan Kaskazini katika mchezo wa robo fainali ya tatu. Polisi Rwanda ilikuwa timu ya kwanza kufuzu kwa hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Atletico Olimpic ya Burundi kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutofungana katika muda wa dakika 90. APR iliwaondoa mahasimu wao wa soka la Rwanda, Rayon Sports kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kufungana mabao 2-2 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Patrick Omog, kocha wa Azam FC tayari ameshafanya maandalizi muhimu kuelekea mchezo wao war obo fainali dhidi ya timu bora ya Merreikh ambayo imeshinda mchezo mmoja tu kati ya mitatu ya hatua ya makundi. El Merreikh ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Pilisi Rwanda katika kundi la Tatu, walichapwa bao 1-0 na Polisi kabla ya kuivurumisha Benadir ya Somalia kwa mabao 4-0 na kulazimishwa sare ya kufunga bao 1-1 na waliokuwa mabingwa watetezi, Vital’o ya Burundi.

Azam FC pia ilimaliza katika nafasi ya pili katika kundi la kwanza baada ya kukusanya pionti nane katika michezo minne. Azam ambao walichukua nafasi ya Yanga baada ya CECAFA kuwaondoa mabingwa hao wa zamani wa Bara, ilianza michuano hiyo kwa kulazimisha suluhu-tasa dhidi ya Rayon Sports, wakaichapa, KMKM ya Zanzibar kwa mabao 4-0, wakalazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Atlabara ya Sudan Kusini, kisha wakamaliza kwa ushindi ‘ mnono’ dhidi ya  ADama City ya Ethiopia.

ROBO FAINALI….

Azam imeruhusu mabao matatu katika michezo minne, wakati El Merreikh wameruhusu mabao mawili katika michezo mitatu iliyopita. Licha ya kufunga mabao kumi ( 10 ) katika michezo minne safu ya mashambulizi ya Azam itatakiwa kuongeza umakini zaidi ili kufuzu kwa nusu fainali. Leonel Saint, Kipre Tcheche, Didier Kavumbangu, John Bocco wote hao wameshafunga katika michuano hii na pengine mshambulizi Bocco anaweza kutwaa tuzo ya ufungaji bora siku ya mwisho ya michuano ikiwa ataendelea kuongeza mabao kutoka katika matatu aliyofunga katika michezo ya hatua ya makundi.

Kavumbagu alitokea benchi na kuisawazishia timu yake wakati ilipolazimishwa sare ya mabao 2-2 na Atlabara, pia alifunga katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ambao alianzishwa mahala kwa Leonel Saint. Washambuliaji hao wanne wamefunga mabao saba lakini wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi za kufunga.

EL Merreikh wameonekana kucheza kwa umakini mkubwa sehemu yao ya ulinzi. Serge Wawa ni mlinzi ambaye hafanyi makosa na hukaba nafasi hadi mwisho. Ili kupata bao/mabao, washambuliaji wa Azam wanatakiwa kucheza kwa umakini zaidi na kujitahidi kufanya vizuri katika kila nafasi itakayotengenezwa na watahitaji kuongeza nguvu zaidi ili kuvunja ukuta wa Wasudan hao ambao upi chini ya mlinzi huyo wa kimataifa wa Ivory Coast.

SAFU YA KIUNGO

Azam ni timu inayofuiatiliwa sana katika michuano hii, kiwango chao kizuri cha uchezaji na mchezo wao wa kasi vimefanya kuwa tishio hadi sasa katika michuano. Safu ya kiungo imekuwa ikitawanya mipira kadri inavyowezekana. Kipre Bolou ambaye anacheza kama kiungo wa ulinzi alifunga bao katika mchezo dhidi ya Atlabara, lakini hatakiwi kusogea hovyo mbele kwa sababu, nahodha wa El Merreikh, Ahmed El Basha ni mchezaji anayepiga pasi za kupenyeza za umbali. Kiungo huyo-mlinzi alifunga bao maridadi wakati timu yake ilipoichapa Benadir anacheza kwa uhakika na ni mchezaji ambaye El Merreikh wanamtumia kama injini ya timu.

Omog anataraji kumpokea kiungo wake Himid Mao ambaye alikosa mchezo wa mwisho wa makundi kutokana na kuwa na kadi mbili za njano. Kurejea kwa Himid kutafanya timu hiyo kuwa na viungo wawili wa uhakika ambao ukabaji wao ni wa kiwango cha juu ili kuendana na kuwazima El Merreikh ambao watakuwa na kiungo mshambulizi,  Mmali, Mohamed Traore. Mchezaji huyo amefunga mabao mawili hadi sasa hucheza kama mshambulizi wa pili lakini hucheza vizuri hadi eneo la katikati ya uwanja kiasi cha kuonekana mata nyingi akicheza kama mchezaji mkuu wa timu.

Kitu muhimu kwa Azam ni kuendelea kutawala mchezo kwa namna yoyote ile huku wakihakikisha hakuna makosa yasiyo na ulazima ambayo yatafanyika. Salum Abubabakary, amekuwa na michuano mizuri sana, lakini uzuri huo utaonekana wakati atakapokutana na wachezaji wenye maarifa na mbinu wa El Merreikh. Kama , Azam itaendelea kumikili eneo hilo la katikati ya uwanja watakuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele.

SAFU YA ULINZI

Allan Wanga amesajiliwa kwa pesa nyingi kutoka AFC Leopards katikati ya mwaka huu, lakini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Kenya ameishia kupoteza nafasi kibao katika michezo mitatu iliyopita. Wanga ameifungia El Merreikh bao moja tu hadi sasa katika michuano hiyo, lakini safu ya ulinzi ya Azam FC haipaswi hata kidogo kumpuuzia na kumuona asiye na madhara. Mechi hii inaweza kumrudisha juu Wanga ambaye licha ya kutofunga ameendelea kucheza vizuri.

Aggrey Morris na David Mwantika itakuwa safu kabambe ya ulinzi ambayo itaweza kumzima mshambuliaji huyo. Shomari Kapombe na Gadiel Michael watacheza katika nafasi za ulinzi wa pembeni na vijana hao wameweka uwiano mzuri katika nafasi hizo ambazo zilikuwa zikiwasumbua Azam kwa muda mrefu. Azam FC imeonekana kuwa na safu imara ya ulinzi lakini si bora kuliko kwa kuwa wachezaji hao hupoteana wakati wanaposhambuliwa mfululizo kiasi cha kucheza kwa presha.

Kitu muhimu katika nafasi hii ni kuzuia mipira ya krosi, kona na faulo kwa namna yoyote ile huku wakiongeza hali yao ya kujiam,ini hata pale mechi inapokuwa ngumu kwa upande wao. Safu ya ulinzi ilipotea kabisa katika mchezo wa sare dhidi ya Atlabara na walionekana kusumbuliwa na mipira ya juu kwa  sababu ya Wasuda hao kuwa warefu zaidi yao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here