Home Utabiri wa Mikeka MATOKEO YA UTABIRI WA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI ILIYOPITA: SHAFFIH DAUDA v...

MATOKEO YA UTABIRI WA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI ILIYOPITA: SHAFFIH DAUDA v ALLEN KAIJAGE NA SUSO ‘COUTINHO’

2810
0
SHARE

MWISHONI mwa wiki iliyopita, ligi kuu soka nchini England ilianza kushika kasi kwa msimu wa 2014/2015.

Mabingwa  wa msimu uliopita, Manchester City, washindi wa pili (Liverpool), washindi wa tatu (Chelsea) na nne  (Liverpool) walianza kwa ushindi katika mechi zao za ufunguzi.

Matokeo ya Manchester United ya kupigwa mabao 2-1 nyumbani Old Trafford dhidi ya Swansea City yalikuwa gumzo duniani kote ikizingatiwa klabu hii ipo chini ya kocha mpya aliyebeba matumaini ya mashabiki wa United, Mholanzi, Louis Van Gaal.

Katika ukurasa wa Utabiri wa Mikeka ndani ya mtandao huu ulifanyika utabiri wa matokeo wa mechi zote zilizopigwa kuanzia jumamosi, jumapili na jumatatu.

Kama ilivyo kawaida ya utabiri huwa kuna kupata na kukosa.

Mtangazaji/Mchambuzi wa soka, Shaffi Dauda na wachambuzi Allen Kaijage na Nicasius Suso ‘Coutinho’ , walitabiri matokeo ya mechi zote za ligi  kuu England.

Jedwali la hapo linaonesha matokeo halisi ya mechi hizo baada ya dakika 90, utabiri wa Dauda na Kaijage. Tafadhali twende pamoja.

MATOKOE YA UTABIRI WA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI ILIYOPITA

JUMAMOSI MATOKEO HALISI DAUDA KAIJAGE SUSA ‘COUTINHO’
Manchester United v Swansea 1-2 4-0 3-0 3-1
Leicester v Everton 2-2 1-3 1-3 1-1
QPR v Hull City 0-1 2-1 1-1 2-1
Stoke v Aston Villa 0-1 1-1 1-1 2-1
West Brom v Sunderland 2-2 1-1 2-1 1-1
West Ham v Tottenham 0-1 1-2 1-2 1-2
Asernal v Crystal Palace 2-1 3-0 3-0 2-0
JUMAPILI        
Liverpool vs Southampton 2-1 5-1 4-0 2-0
Newcastle v Manchester City 0-2 2-4 0-3 0-3
JUMATATU        
Burnley v Chelsea 1-3 1-3 0-2 0-2
       

 

Katika utabiri huu, Shaffih Dauda aliweza kupatia mchezo wa Chelsea siku ya jumatatu ambapo matokeo ya 3-1 ambayo Jose Mourinho alipata ugenini dhidi ya Burnley yalikuwa sawa na utabiri wake.

Kaijage na Suso walichemsha mechi zote. Endelea kufuatilia mtandao huu katika utabiri wa ligi mbalimbali barana Ulaya na hata ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here