Home Kimataifa TAKWIMU: BRAZIL INAONGOZA KUUZA WACHEZAJI KATIKA SOKO LA KIMATAIFA LA USAJILI DUNIANI

TAKWIMU: BRAZIL INAONGOZA KUUZA WACHEZAJI KATIKA SOKO LA KIMATAIFA LA USAJILI DUNIANI

900
0
SHARE

Brazil inaongoza kujihushisha na usajili wa kimataifa kwa mpira wa miguu tangu FIFA TMS ianze kukusanya taarifa za usajili kutoka nchi wanachama duniani kote mwezi Oktoba 2010.

Pia wachezaji wa Brazil ndio wanaongoza kuuzwa katika soka la kimataifa la usajili.

Hapa kufafanua namna Brazil inavyojihusisha katika dirisha la usajili la kimataifa kwa kuzihusisha klabu za nchi hiyo na wachezaji wake kwa miaka mitatu iliyopita.

  • Kulikuwa na dili 5,003 katika soka la usajili zikihusisha klabu za Brazil kati ya januari 2011 na Juni 2014, ni namba kubwa zaidi duniani.
  • Katika dili 5,526 za usajili, wachezaji wa Brazil ndio walihamishwa zaidi duniani kote kati ya Januari 2011 na Juni 2014. Hii ni zaidi ya mara mbili dhidi ya taifa la Argentina ambalo linashika nafasi ya pili kwa kuuza wachezaji wengi  ambapo wachezaji 2,632 walihamishwa.
  • Ikiwa imebalansi vizuri ada ya uhamisho iliyokuwa dola za kimarekani 579 kati ya januari 2011 na juni 2014, klabu za Brazil ziliweka rekodi ya kupokea dili kutoka kwa kila taifa katika soko la usajili.
  • Ureno ni nchi inayofungua milango ya wachezaji wengi wa Kibrazil kwenda Ulaya, ambapo wachezaji 805 walihamishwa baina ya mataifa haya kati ya januari 2011 na juni 2014, hii ndio idadi kubwa zaidi ya wachezaji kuhusisha mataifa mawili duniani kote.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here