Home Kitaifa MFARANSA WA SIMBA SC ‘BABU’ PATRICK LIEWIG ATUA NCHINI KUINOA MTIBWA SUGAR

MFARANSA WA SIMBA SC ‘BABU’ PATRICK LIEWIG ATUA NCHINI KUINOA MTIBWA SUGAR

786
0
SHARE

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

TAARIFA za mchana huu zinaeleza kuwa aliyekuwa kocha mkuu wa Simba sc, Mfaransa, Patrick Liewig amerejea nchini kwa mara ya pili na kujiunga na Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa meneja wa kocha huyo, Abdulfatah Salim Saleh, Mfaransa huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwanoa mabingwa hao wa zamani wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000.

Mtibwa Sugar ilivutiwa na utendaji wa Liewig akiwa Simba kabla ya kufukuzwa mwaka juzi na nafasi yake kuchukuliwa na mzawa, Abdallah Kibadeni ambaye naye alifukuzwa baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa mzunguko mmoja msimu wa 2012/2013.

Baada ya kutimuliwa na Simba, Liewig alikuwa anatajwa kuwania na Coastal Union, lakini taarifa hizo hazikutimia kwa wakati huo.

Hata hivyo haijaelezwa hatima ya kocha wa sasa wa Mtibwa Sugar, Mzalendo Mecky Mexime ambaye ana mipango kabambe ya kuirudisha timu hiyo katika soka la ushindani nchini.

Mtibwa Sugar ni moja ya klabu kongwe nchini Tanzania na inaendeshwa kwa mfumo wa kampuni sawa na Kagera Sugar na Azam fc.

Kurejea kwa Liewig nchini kutaongeza uhondo wa ligi kuu kwasababu idadi ya makocha wa kigeni imeongezeka.

Yanga wananolewa na Mbrazil, Marcio Maximo, wakati Simba wao wamemuajiri Mzambia Patrick Phiri siku chache baada ya kumtimua Mcroatia, Zdravko Logarusic maarufu kwa jina la Loga.

Mabingwa, Azam fc wananolewa na Mcameroon, Joseph Marius Omog wakati Mtibwa wao wameamua kumchukua Mfaransa Liewig.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here