Home Utabiri wa Mikeka   KAIJAGE Vs SUSO NDANI YA LIGI KUU SOKA NCHINI ENGLAND LEO

  KAIJAGE Vs SUSO NDANI YA LIGI KUU SOKA NCHINI ENGLAND LEO

1423
0
SHARE

                                                               

                                            MANCHESTER UNITED Vs SWANSEA

Utamu wa hii mechi upo sehemu tatu kuu. Uwepo wa Van Gaal, Kiwango cha mechi za maandalizi ya ligi, na nahodha Rooney. Vyote hivi vinasubiriwa kwa hamu kabisa na mashabiki wa Manchester united. Hawajapoteza mechi  yoyote ya maandalizi, hii nadhani ni nguvu kubwa kuliko lolote itawahamasisha sana. Na kama Kuna usajiri mkubwa nadhani ni Van Gaal. Hata waje Di Maria na Vidal huyu atabaki kuwa usajiri mkubwa wa Man U. Imani yote ipo kwa huyu na pia tunaweza kumuona Rooney mpya sasa. Upande wa pili Kuna Gomis, nadhani Ndo jina jipya linaloweza kuleta tabu sana. Umbo lake na Bony ni silaha ambazo Man u  inabidi wazichunge. Unaweza kuiita mechi bora ya jumamosi kutokana na ilivyovibeba. Nawaona wote wakipata magoli, na haswa kama Van Gaal akitumia 352 kwa mchezo wa Swansea ni rahisi kuufungua huu mfumo

SUSO         Manchester united 3-1 Swansea

KAIJAGE    Manchester united 3-0 Swansea                            

                  

                                       WEST BROMWICH ALBION Vs SUNDERLAND

Timu hizi zilipambana vilivyo msimu uliopita kujinusuru na janga la kushuka daraja.westbromwich watakua wakifurahia huduma ya mshambuliaji wao mpya raia wa Nigeria Brown ideye,mshambuliaji huyo ambaye alivunja rekodi ya usajili ya westbromwich kwa mara ya kwanza atakanyaga nyasi za uwanja wa hawthorns huku mashabiki 27000 wakiwa nyuma yake.Pia kiungo craig gadner atakuwa uwanjani kwa mara ya kwanza akiikabili timu yake ya zamani,wakati huo huo beki mkongwe joleon lescott atakuwa nje ya kikosi hicho akiendelea kuuguza majeraha yake.

Kwa upande wao sunderland watamkosa kiungo wao muhimu raia wa italia giaccherini lakini watakuwa wakifurahia huduma ya kiungo wao mpya mwenye kipaji  jack rodwell.Mtihani mkubwa kwa kocha guss poyet utakua juu ya na nani anze kulinda lango kati ya vito mannone na kipa mrefu kutoka Manchester city carlos pantilimon.

KAIJAGE  west bromwich 2-1 sunderland

SUSO       west bromwich 1-1 sunderland

 

                                                   STOKE  Vs ASTON VILLA

Mechi nyingine nzuri ambayo Sio mbaya ukiitizama, tofauti ndogo iliyopo baina ya hizi timu mbili ni kwamba Stoke ni wazuri zaidi kwa mipira mirefu. Msimu uliopita walikuwa na wastani wa futi 6. Silaha kubwa pamoja na ongezeko la Bojan hawa Stoke ni,uwanja wa nyumbani. msimu uliopita ni moja ya timu zilizopoteza mechi chache zaidi wakiwa nyumbani. Wakati Aston Villa wakimkosa Benteke silaha Yao itakuwa Agbonlahor. Joe Cole na Bent Sio wa siku zote tena. Uwepo wa Crouch pia utakuwa silaha.

SUSO         stoke 2-1 villa
KAIJAGE   stoke 1-1 villa

                   

                                                      QPR Vs HULL CITY

Kwa mara nyingine tutashuhudia qpr na kocha wake harry rekdnap ndani ya ligi kuu England.QPR kwa mara nyingine watashuka uwanjani kuwakaribisha makamu bingwa wa kombe la fa hull city.QPR wataongozwa na mshambuliaji wao roic remy,mshambuliaji huyo  awali alifeli vipimo katika harakati zake za kujiunga na Liverpool.Kiungo mtukutu Adel taarabt ataikosa mechi hiyo muhimu ya ufunguzi wa ligi.Beki mkongwe kutoka Manchester united  rio Ferdinand anatarajiwa kuanza mechi hiyo huku kocha rekdnapp akitarajia kutumia mfumo wa beki wa kati watatu ili kukizi kasi ya beki rio ferdinand

Hull city wao watashuka dimbani huku wakikumbuka mafanikio yao waliyoyapata msimu uliopita.Hull city wataendelea kuwategemea viungo wao maridadi Livermore na huddlestone ili kupata matokeo chanya.Ukiacha Manchester united QPR  na westbromwich  kocha bruce nae ni muumini wa catenacio,nae anatarajiwa kutumia mabeki watatu nyuma

KAIJAGE  QPR 1-1 hull city

SUSO        QPR 2-1 hull city

                                                            LEICESTER vs EVERTON

Naamini hata wao wanajua kwa ugeni huu hii ni moja ya mechi ngumu sana kwao japo wapo nyumbani. Everton ni moja ya timu zilizoupeleka msimu puta sana. Leicester Sio wabaya wanavyojipanga  na kucheza inawapa nafasi ya kupigana katika ligi hii. Nadhani kabla hawajapata dhoruba na kuchoka na ligi hizi ni mechi ambazo huwa timu zinaitua ligi. Lakini kwa kiwango na Kasi aliyotengeneza Martinez na sasa Ana uhakika na huduma za Barkley na Lukaku atawapa shida.
Leicester Sio wa kudharau wameshinda zaidi ya mechi tano kwenye mechi za maandalizi.
SUSO         Leicester 1-1 everton

KAIJAGE    Leicester 1-3 everton

                                     WEST HARM Vs SPURS

London derby.Hizi ni timu zenye mashabiki wengi zaidi kwenye jiji la London.Mara zikutanapo nyasi lazima ziwake moto.msimu uliopita washabiki wa spurs walikua si kitu mbele ya wagonga nyundo wa London.Hizi mechi mara nyingi huwa na matokeo ya kustaajabisha.Timu unayofikiri bora ikifungwa wala usishangae.Mechi hii inafanana na sunderland na newcastle au Liverpool na everton,ukiamka vizuri utashinda mechi  na ukiamka vibaya lazima udondokee pua.

Silaha ya spurs itakua ni kocha wao mpya pochettino ambaye ni muumini wa soka la kuvutia huku west ham ambayo ni moja ya  timu zenye ulinzi usiopitika kirahisi itamtegemea zaidi mshambuliaji wake mpya kutoka argentina Mauro zarate.

KAIJAGE  west ham 1-2 spurs

SUSO       west ham 1-2 spurs

     

                                                ARSENAL Vs PALACE

Wakati  crystal palace wakiwa na huzuni kwa kuondokewa na kocha wao kipenzi aliyewafikisha kwenye nafasi ya juu zaidi katika historia ya klabu hiyo(nafasi ya 11) Arsenal kwa upande wao watakua na furaha tele na mioyo yenye shauku kumshuhudia nyota wao mpya alexis sanchez akicheza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu uingereza.

Crystal palace walio chini ya uangalizi wa kocha keith millen wanahitaji nguvu ya ziada ili kuondoka na angalau pointi moja katika uwanja wa emirates

KAIJAGE  arsenal 3-0 palace

SUSO        arsenal 2-0 palace

 

                                            LIVERPOOL vs SOUTHAMPTON

Kwa haraka Tu, hii waweza kuita match of the weekend au mechi ya wikiendi hii. Liverpool ina wachezaji watatu waliokuwa chachu ya mafanikio ya Southampton msimu uliopita. Hii tayari ni upinzani wa kukupa hamasa ya kutizama nini watafanya. Wakati Liverpool wakifurahia rekodi Yao nyumbani msimu uliopita Southampton ilikuwa ya kwanza kuwafunga hapo. Tatizo la Liverpool msimu uliopit lilikuwa beki, na ndio lililowanyima ubingwa uliokuwa unawezekana, ndio maana si ajabu kasajili mabeki watatu mpaka sasa.  Sasa ni Southampton mpya na Liverpool inayomkosa Suarez. Scherneiderlin mchezaji muhimu kwangu Southampton naye hataki kucheza. Koeman Ana kazi ya kuwatuliza mashabiki. Rodgers Ana kazi ya kuwahaminisha mashabiki amefanya usajiri sahihi. Inawezekana hii isiwe Liverpool itakayofunga magoli mengi kama msimu uliopita ila naiona kama itakuwa nyepesi na hatari zaidi.

SUSO      Liverpool 2-0 southampton

KAIJAGE   Liverpool 4-0 southampton

 

                                        NEWCASTLE UNITED vs MANCHESTER  CITY

Huku kaondoka Remmy huku kaongezeka Mangala.Newcastle wamepunguza mshambuliaji , Man City wameongeza beki. Pamoja na kupoteza mechi dhidi ya Arsenal bado Man City wana nguvu kupita maelezo. Kinachosubiriwa kwa hamu ni ukuta huu kwa sasa wa Kompany na Mangala. Sidhani kama Newcastle watakuwa tayari kupigania nafasi sita za juu mpaka sasa,  ingawa watakuwa ni moja ya timu za kuzifikiria Mara mbili. Ni mechi ngumu lakini inayoweza kuleta matokeo ya ajabu.
SUSO       Newcastle united 0-3 manchester city

KAIJAGE  Newcastle united 0-3 manchester city
                                       BURNLEY Vs CHELSEA

Umeshawai sikia stori kuhusu mashabiki vichaa duniani? Kama bado usilale siku ya jumatatu ili uwashuhudie mashabiki vichaa wa burnley .Burnley wanaamini kocha wao sean dyche ni kocha bora kuliko kocha wa Chelsea morinho.Wanaamini pesa anazotumia morinho kwenye usajili angepewa dyche angekua na mafanikio kuliko morinho.kumbuka timu ya burnley ni miongoni mwa timu zilizokuwa na bajeti ndogo lakini ikafanikiwa kupanda daraja huku mtaji wao mkubwa ukiwa umoja ulioundwa na kocha dyche pamoja na sapoti ya mashabiki vichaa wa burnley

Chelsea itawakaribisha nyota wao wa timu ya taifa ya Hispania Diego Costa na Cesc Fabregas ambaye anatarajiwa kuziba vilivyo pengo la Frank lampard ambaye wengi wanaamini kuwa ndie mchezaji bora wa muda wote wa Chelsea.

KAIJAGE  burnley 0-2 chelsea

SUSO      burnley 0-3 chelsea 

 

Imeandaliwa na

Allen Kaijage 0655 106767

             Na

Nicasius Suso 0712203770

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here