Home Kimataifa TATA MARTINO KOCHA MPYA WA ARGENTINA.

TATA MARTINO KOCHA MPYA WA ARGENTINA.

832
0
SHARE

Kocha wa zamani wa Barcelona Gerardo Martino amechaguliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina mara baada ya kocha aliyeifikisha fainali ya kombe la dunia Alejandro Sabella kujiuzuru mara tu baada ya kufungwa bao 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya mwaka 2014.
Martino alisitishiwa huduma kwenye klabu ya baada ya kuwa na msimu mbaya huku akiiongoza Barcelona kumaliza msimu bila taji lolote kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.
Uzoefu akiwa na Paraguay.
Martino mwenye umri wa miaka 51 ana uzoefu wa kufundisha soka akiwa ameiongoza timu ya taifa ya Paraguay kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kati ya mwaka 2006 hadi 2011,Martino atatangazwa rasmi siku ya Alhamis hii ya tarehe 14 August.
Akiwa kocha wa Barcelona aliiongoza timu hiyo kushinda michezo 40 kati ya michezo 59.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here