Home Dauda TV liverpool itamaliza nje ya top 4 msimu huu.

liverpool itamaliza nje ya top 4 msimu huu.

882
0
SHARE

ambapo vilabu mbali vitashuka dimbani kuanza harakati mbali mbali,baadhi vikiwania ubingwa,vingine vikipambana kubaki ligi kuu na vingine vikipigana kumbo kutoshuka daraja.

Msimu uliopita tulishuhudia klabu ya Liverpool ikileta changamoto kubwa kwenye ligi kuu ya England na kumaliza nafasi ya pili huku ikizidiwa pointi mbili tu na waliokuwa mabingwa, Manchester City .
Msimu huu siwapi nafasi Liverpool ya kumaliza ndani ya top 4 kutokana na sababu kadhaa,miongoni mwa sababu hizo ni kuondoka kwa mshambuliaji Luis Suarez ambaye msimu uliopita alifunga jumla ya mabaoa 31 kwenye ligi kuu ya England,Suarez msimu huu amejiunga na FC Barcelona ya nchini Hispania.
Sababu nyingine ni kitendo cha Liverpool kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani ulaya huenda kikaipelekea kushindwa kushiriki kwa ufanisi kwenye ligi kuu na kupelekea kuipa nafasi Man Utd kufanya vizuri kwasababu haitakuwa na mashindano mengi msimu huu baada ya kushika nafasi ya saba msimu uliopita.
Kwaiyo timu ninazozipa nafasi ya kushika nafasi nne za juu ( bila mpangilio maalum ) hadi kufika mwishoni mwa msimu ujao wa 2014/2015 ni:

Arsenal
Manchester City
Chelsea
Manchester Utd.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here