Home Dauda TV DIAMOND PLATNUM- ”MRISHO NGASSA NDIYE MWANASOKA PEKEE NINAYEMFAHAMU TANZANIA”

DIAMOND PLATNUM- ”MRISHO NGASSA NDIYE MWANASOKA PEKEE NINAYEMFAHAMU TANZANIA”

2626
0
SHARE

Mwanamuziki wa Bongo Flovour Nchini Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinums, amesema hajaridhilika na alipo sasa kimuziki, ndio maana kila siku anajifunza kwa kufuatilia kwa ukaribu maisha ya Nyota wengi hasa wanamichezo Kutoka Mataifa Tofauti Duniani.

ETOO
Diamond ambae ni miongoni mwa wanamuziki waliofanya vyema kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta Mkoani Mwanza hivi karibuni, ametoa taarifa za kuwafuatilia nyota hao mbalimbali kwenye mahojiano maalum na Shaffih Dauda, kupitia Dauda TV.
Miongoni mwa nyota ambao Diamond anawafuatilia hasa kupitia Mtandao wa Instagram, ni Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon Samuel Etoo, Kiungo Mshambuliaji wa Brazil na Barcelona Neymar, Bondia Mmarekani Floyd Myweather na wengineo.

DROGBA
Pamoja na Diamond kuweka hilo wazi, pia amesema aliwahi kucheza masumbwi, kisha akahamia kwenye Soka hasa nafasi ya golikipa na namba sita yaani kiungo Mkabaji, lakini aliamua kuachana na Soka baada ya mama yake kumsii kufanya hivyo kwa muda mrefu.

Awali kulikuwa na hisia kwamba Diamond anashabikia timu ya Dar-es-salaam Young Africans, hasa baada ya kuweka picha kwenye mitandao akiwa na Mrisho Ngasa mara kadhaa, lakini amesema yeye na Ngasa ni marafiki, na sio mshabiki wa Yanga kama inavyodhaniwa.

FLOYD MAYWEATHE
Diamond ameongeza kwa kusema sio tu haishabikii Yanga, bali kwa hapa nyumbani hana timu anayoishabikia, badala yake anaipenda FC Barcelona ya Hispania, ambapo amesema kunakipindi mapenzi yalizidi kwa timu hiyo, kiasi cha kuweza kupanga kikosi chote.
dauda Diamond

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here