Home Kitaifa COASTAL UNION KUKIPIGA NA HANDENI CITY JUMAMOSI DIMBA LA AZIMIO

COASTAL UNION KUKIPIGA NA HANDENI CITY JUMAMOSI DIMBA LA AZIMIO

972
0
SHARE

Na Mwandishi wetu, Tanga
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dr.Abdallah Kigoda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya kirafiki kati ya timu ya vijana ya Coastal Union na Handeni City utakaochezwa Jumamosi wiki hii wilayani humo.
Mchezo huo ni moja kati ya mechi mbalimbali za majaribio wanazocheza timu hiyo lengo likiwa ni kukipa makali kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana ikiwemo Rolling Stone na mengine yatakayojitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Salim Bawazir alisema mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa soka Kigoda ambao awali ulikuwa ukiitwa Azimio kuanzia majira ya saa kumi jioni.
Bawaziri timu hiyo itaondoka wilaya ya Tanga Jumamosi asubuhi ili kuweza kufika mapema wilayani humo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi hiyo ikiwemo kuwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi.
“Mchezo huu ni muhimu sana kwa timu yetu ya vijana kwani wanajiandaa na mashandano mbalimbali hasa yale ya vijana ikiwemo Rolling Stone na Kombe la Uhai Cup “Alisema Bawaziri .
Katika hatua nyengine wachezaji wa waliosajiliwa kwenye timu ya Coastal Union ambayo inashiriki mashindano ya ligi kuu Tanzania bara wanatarajiwa kuwasili mkoani Tanga muda wowote kuanzia jana.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here