Home Maajabu ya Brazuka Pekerman apata kura 400,000 za Uraisi pamoja na jina lake kutokuwa miongoni...

Pekerman apata kura 400,000 za Uraisi pamoja na jina lake kutokuwa miongoni mwa wagombea.

974
0
SHARE

Jose Pekerman amepata jumla ya kura 400,000 kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua raisi wa nchi ya Colombia pamoja na kutokuwa miongoni mwa majina ya wagombea.

Maelufu ya wapiga kura nchini humo waliamua kuaribu kura zao kwa kumchagua kocha huyo wa kikosi cha timu ya taifa ya Colombia ili kuonyesha ni jinsi gani wanamkubali,

josePekerman ambaye ni raia wa Argentina aliwafurahisha mashabiki wa soka nchini Colombia baada ya kukiongoza kikosi chake kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Ugiriki katika wiki ambayo wakazi wa nchi hiyo walikuwa kwenye mchakato wa kupiga kura za kumchagua raisi wa nchi yao.

Wacolombia zaidi ya 100,000 walivuka boda na kuingia mjini Belo Holizinte uliopo mashariki mwa nchini Brazil kushuhudia mpambano huo lakini pia kupata fursa ya kunywa pombe kwasababu sheria za Colombia zinazuia unywaji wa pombe nchini humo katika lile juma ya upigaji kura.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here