Home Dauda TV KAMPUNI YA BIN SLUM YAINGIA MKATABA WA MILIONI 50 NA STENDI UNITED

KAMPUNI YA BIN SLUM YAINGIA MKATABA WA MILIONI 50 NA STENDI UNITED

1125
0
SHARE

 

Baada ya kuingia mkataba na Mbeya city kampuni ya Bin Slum haijasimama kendelea kutoa support ya uhakika kwenye mpira wa Tanzania. Hivi sasa waliofaidika na udhamini wa kampuni ya Bin Slum ni Stendi united ambao wamesaini mkataba wa milioni 50.

Mkurugenzi wa kampuni ya Bin Slum bwana Nassor Bin Slum amesema kwamba kama kawaida ya kampuni ya Bin Slum ni kusaidia mpira wa Tanzania hasa timu zinakua na kufanya vizuri wameendelea kufanya hivyo kama ilivyokuwa kwa Mbeya city.

Nassor Bin Slum amesema kwamba milioni hizi 50 kwa Stendi United ni changamoto kwao na kampuni inaweza kuongeza mkataba mnono msimu ujao kama timu ikionyesha mwelekeo mzuri.

Stendi united watavaa jezi zenye logo ya Double Star Tire, mwenyekiti stendi united bwana Amani Vicent ametoa shukrani na kuahidi timu haitamuangusha mdhamini.

Pia mlezi wa Stendi united mbunge wa Shinyanga mjini bwana Stephen Masele ametoa shukrani zake na kusema kwamba timu yake inajiandaa vema ikiwemo kuimarisha timu ya vijana.


 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here