Home Kimataifa JOEL CAMPBELL ATAPEWA NAFASI ASERNAL, WENGER AMETHIBITISHA

JOEL CAMPBELL ATAPEWA NAFASI ASERNAL, WENGER AMETHIBITISHA

1168
0
SHARE

 Joel Campbell aliisaidia Costa Rica kuibamiza  Uruguay siku ya jumamosi.

KOCHA Arsene Wenger yuko tayari kumpa fursa Joel Campbell ya kuichezea Asernal.
Kocha huyo wa Asernal ambaye yupo mjini Porto Alegre kama mtangazaji wa Televisheni ya Ufaransa, jumapili jioni alishuhudia Ufaransa ikichapa Honduras maao 3-0.
 Lakini Wenger amethibitisha kuwa amepanga kumrudisha tena katika kikosi cha Asernal nyota huyo wa  Cost Rica ambaye alifanya kazi nzuri wakiizamisha Uruguay.
Kocha huyo mnamo mwaka 2011 alimtoa kwa mkopo nyota huyo mwenye miaka 21.
Who's the daddy? Campbell celebrates after scoring Costa Rica's equaliser early in the second half

 Campbell akishangilia bao lake la kusawazisha

 ‘Hakika atarudi kwetu wakati wa maandalizi ya msimu,” Wenger aliwaambia Sportsmail. “Ameimarika vizuri”.
 
Wenger iliikosa mechi ya Costa Rica kwasababu alisafiri kwenda Porto Alegre, lakini alipokea ujumbe kutoka kwa kocha wa zamani wa Chelsea Avram Grant, ambye yuko na luninga ya Israel akimtaarifu jinsi ambavyo Campbell alicheza vizuri.
Campbell aliifungia Costa Rica bao moja na kutengeneza nafsi moja katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uruguay mjin Fortaleza.
Campbell alisaini mkataba na Asernal miaka mitatu iliyopita, lakini muda mrefu amecheza kwa mkopo , lakini Wenger anahisi sasa imefika muda muafaka wa kumrudisha katika timu ya kwanza ya klabu yake.
 
 Mara ya kwanza alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Lorient nchini Ufaransa, halafu Real Betis nchini Hispania na  kwasasa anaichezea timu ya Ugiriki ya  Olympiacos, ambapo amewavutia  Manchester United katika michuano ya ligi ya mabingwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here