Home Maajabu ya Brazuka Foleni ndefu ya kuingia uwanjani yawachelewa mashabiki kuwahi mechi…

Foleni ndefu ya kuingia uwanjani yawachelewa mashabiki kuwahi mechi…

1145
0
SHARE

IMG-20140616-WA0024 IMG-20140616-WA0025 IMG-20140616-WA0028 IMG-20140616-WA0029   IMG-20140616-WA0017 IMG-20140616-WA0019

BRASILIA, Brazil – Maelfu ya mashabiki walikosa sehemu ya mchezo ambao Uswizi iliifunga Ecuador mabao 2-1 kwenye jiji la Brasilia ambao pia ndio makao makuu ya nchi ya Brazil.

Sababu iliyopelekea mashabiki hao kuchelewa kuingia uwanjani ni foreni ndefu kabla ya kupita eneo la usalama.

Mashabiki waliokuwa na tiketi za kuushuhudia mchezo huo walichelewa karibia nusu saa kuingia uwanjani ambapo baadhi yao hawakufanikiwa hata kuliona bao la kuongoza la Ecuador lililofungwa kwenye dakika 22.

Hakukuwepo taarifa kutoka kwenye mamlaka husika ya kuelezea nini kilikuwa chanzo cha kuchelewa mashabiki kupita kwenye eneo la usalama.

Siku chache kabla ya michuano hii kuanza maafisa wa FIFA waliwataka mashabiki kuwahi mapema viwanjani ili kuweza kukaguliwa mapema kabla ya michezo kuanza.

Hata hivyo mashabiki wote waliokuwa na tiketi walifanikiwa kuingia uwanjani hapo kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here