Home Kimataifa SIMBA WASIOFUGIKA CAMEROON WAANZA VIBAYA KOMBE LA DUNIA, WACHAPWA 1-0 NA MEXICO,...

SIMBA WASIOFUGIKA CAMEROON WAANZA VIBAYA KOMBE LA DUNIA, WACHAPWA 1-0 NA MEXICO, WAAMUZI TENA…

827
0
SHARE
  Oribe Peralta (kushoto) aliwafungia Mexico bao pekee la ushindi katika dakika ya 61.
BAO pekee la Oribe Peralta katika dakika ya 61 limetosha kuwapa Mexico ushindi wa mechi ya kwanza ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil, lakini bado waamuzi wameonekana kuzua hofu kiuwezo
Mwamuzi  kutoka Colombia, Wilmar Roldan aliwanyima mabao mawili Mexico katika dimba la  Natal Estadio das Dunas kipindi cha kwanza baada ya kutoa maamuzi ya kuotea kwa mfungaji wa mabao hayo, mchezaji wa zamani wa Tottenham Giovani dos Santos.
Lakini mambo yalikuwa nafuu kwa Mexico waliotawala mchezo huo baada ya mlinda mlango wa Cameroon Charles Itandje kuutema mpira uliopigwa na Dos Santos na ukamkuta Peralta akiwa katika nafasi nzuri ambapo hakufanya makosa na kuukwamisha mpira nyavuni.
Matokeo hayo yanawapa nafasi nzuri  Mexico kufuzu hatua ya 16 bora kutoka kundi A sambamba na wenyeji Brazil na timu hizo zitaumana jumanne ya wiki ijayo mjini

 Fortaleza.

Ahead: Peralta wheels away in celebration after given Mexico a deserved lead in the Group A clash

Peralta akishangilia bao lake
Jubilant: The Mexico players celebrates the opening goal with the substitutes on the sidelines

 Wachezaji wa Mexco wakishangilia bao lao usiku huu.
Bad day: Giovani Dos Santos saw two seemingly fair goals disallowed during the first half

 Siku mbaya: Giovani Dos Santos alishuhudia mabao yake mawili yakikataliwa

 

Kikosi cha Mexico leo: Ochoa, Layun, Moreno, Marquez, Rodriguez, Aguilar, Guardado (Fabian 69′), Vazquez, Herrera, Giovani, Peralta (Hernandez 74′).
Wachezaji wa akiba: Corona, Salcido, Reyes, Jimenez, Pulido, Ponce, Brizuela, Aquino, Pena, Talavera.
Kdi ya njano: Moreno
Goli: Peralta 61′

Kikosi cha Cameroon: Itandje, Djeugoue (Nounkeu 45′), N’Koulou, Chedjou, Assou-Ekotto, Song (Webo 79′), Mbia, Enoh, Moukandjo, Eto’o, Choupo-Moting.

Wachezaji wa akiba: Feudjou, Aboubakar, Makoun, Bedimo, Fabrice,
Salli, Matip, Nyom, N’Djock.
Kdi: Nounkeu

Mwamuzi: Wilmar Roldan Perez
Idadi ya mashabiki: 39, 216
One to forget: Samuel Eto'o missed a glorious chance to give his side the lead in the first half

 Samuel Eto’o alikosa nafasi ya kuifungia bao Cameroon kipindi cha kanza.
Bad call: Dos Santos (right) puts the ball in the net again but the goal was disallowed due to an offside

 Dos Santos (kulia) akifunga bao la pili lakini nalo lilikataliwa na mwamuzi
Still singing? Spectators sit under pouring rain as they watch the Group A match

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here