Home Kimataifa BRAZIL; WAFALME WA KANDANDA DUNIANI, WENYE MFUNGAJI WA KOMBE LA DUNIA

BRAZIL; WAFALME WA KANDANDA DUNIANI, WENYE MFUNGAJI WA KOMBE LA DUNIA

2424
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole
Brazil ilipata ushindi muhimu na wa kuvutia baada ya kutoka nyuma ya goli 1-0, na kushinda kwa magoli 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa fainali za kombe la dunia usiku wa kuamkia leo. Mlinzi wa kushoto wa Selecao, Marcelo alijifunga wakati akijaribu kuzuia mpira uliotoka katika upande wa kushoto.
Mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa Croatia, Niko Kovac alisema kuwa mwamuzi alionekana kuipendelea Brazil ila akawasifu vijana wake kwa kuanza kuongoza mechi. Goli la mapema la kujifunga la wenyeji liliwashtua mashabiki wa Brazil, kwani Croatia ilikataa kuingia katika mtego wa samba.
Croatia waliukimbiza mpira na wachezaji wakawa na mchezo wa kasi, Brazil ilijaribu kutaka kupunguza presha ya mashabiki wake kwa kucheza mpira wa uhakika wa taratibu lakini wakajikuta katika wakati mgumu kwa sababu wapinzani wao walikimbia sana uwanjani. Neymar alipata kadi ya njano ya kwanza katika michuano ya mwaka huu, ila akachomoza na kung’ara katika mchezo huo. Alifunga goli la kusawazisha akimalizia pasi safi ya kiungo, Oscar na kuifanya Brazil kwenda mapumziko wakiwa sare ya kufungana goli 1-1.
Goli la pili la Brazil lilitokana na mkwaju wa penalty baada ya mshambulizi Fred kuangushwa katika eneo la hatari, na Neymar akicheza mchezo wake wa kwanza wa fainali za kombe la dunia alijiamini na kupiga mkwaju mkali ambao kipa wa Croatia, Stipe Pletikosa alijaribu kuufuata bila mafanikio. Goli hilo la dakika ya 71 lilitosha kuwafanya wenyeji kujiamini. Paulinho ambaye kabla ya kuanza kwa michuano alionekana kushuka kiwango chake, aliweza kuichezesha Brazil kwa kushirikiana na Oscar na mechi ikaanza kuwa ngumu kwa Croatia.

article-2656584-1EB59B0F00000578-301_634x422Marcelo akijifunga goli katika mchezo wa jana.

Katika dakika 20 za mwanzo Croatia ilionekana kutawala eneo la katikati ya uwanja lakini wakajikuta wakiishiwa pumzi na pale walipojaribu kufikiria cha kufanya wakajikuta wakiingia katika mbinu za Brazil. Mabadiliko ya kwanza yaliyofanywa na kocha Big Phill yalikuwa ni kumtoa, Paulinho na kumuingiza uwanjani kiungo Hernanes katika dakika ya 63, na dakika tano baadae akampumzisha Hulk na kumuingiza uwanjani, Bernard yalikuwa ni mabadiliko ambayo yaliifanya Brazil kucheza mchezo wa kasi kwa lengo la kupata goli la pili na jambo hilo lilileta mafanikio baada ya Neymar kufunga goli dakika ya 71.

Walinzi wa Croatia Vedran Corluka na Dejan Lovren walipata kadi za njano katika dakika za 66 na 69 baada ya mechi kuanza kuwa ngumu kwa upande wao. Ukitoa goli la kujifunga la Marcelo, safu ya ulinzi ya Selecao ilikuwa imara na ushirikiano wa David Luiz na nahodha, Thiago Silva ulikuwa mzuri. Croatia walipata goli pekee baada ya krosi kutoka katika upande wa Dan Alves na tatizo la walinzi wa pembeni lilionekana kuwasumbua wakati Fulani Brazil.

Brazil walicheza faulo tano tu wakati Croatia ilicheza faulo 21. Hiii ni ishara kuwa mechi ilikuwa ngumu kwa Croatia ambao walipiga mashuti 10 na ni mashuti manne tu yaliyolenga goli. Brazil walipiga mashuti 14 na tisa yalikwenda langoni, walistahili kufunga magoli matatu katika mchezo wa jana, hasa ukizingatia kuwa walimiliki mpira kwa asilimia 58, kupata kona saba na kuotea mara moja.

article-2656584-1EB5911E00000578-791_634x377Neymar akionesha ufundi wake katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Croatia jana usiku

Mara nne. Golikipa Julio Cesar aliiokoa timu isifungwe hiyo inaonesha kuwa wasipokuwa makini wanaweza kuanguka katika siku za mbele. Mashambulizi sita ya uhakika yaliokolewa na kipa, Stipe ni kigezo tosha kinachoweza kunishawishi kuamini kuwa Brazil ni timu iliyokamilika na i9nayoweza kutwaa ubingwa wa kombe hilo mwaka huu. Ukitoa bkigezo cha kucheza nyumbani ambako hamasa kubwa wanaipata kutoka kwa wananchi wao kama ilivyotokea mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana, Selecao ipo vizuri katika nafasi ya ulinzi, nafasi ya kiungo na tayari safu ya mashambulizi imempata mfungaji wa kombe la dunia, si mwingine ni Neymar.

article-2656584-1EB5ACDC00000578-109_634x290Neymar akimpiga kiwiko Luca Modric na aliambulia kadi ya njano.

Kufunga magoli mawili katika mchezo wa kwanza tu wa fainali hizo tena akiwa na umri wa miaka 21 ni kitu ambacho kinamtambulisha tofauti na washambuliaji wanaotazamwa sana, Cristiano Ronaldo, Leonel Messi na Wayne Rooney ambao hakuna kati yao aliyefunga magoli matatu katika historia ya michuano hiyo japo wote wameshashiriki mara mbili katika fainali za miaka ya 2006 na 2010. Brazil, wafalme wa kandana duniani wanaoweza kutwaa ubingwa wa kwanza wa dunia katika ardhi ya nyumbani.
0714 08 43 08

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here