Home Tetesi za Usajili BRAZIL 1 vs 0 SERBIA: FRED AWAOKOA, LAKINI MASHABIKI WAZOMEA KIWANGO `MBOFU...

BRAZIL 1 vs 0 SERBIA: FRED AWAOKOA, LAKINI MASHABIKI WAZOMEA KIWANGO `MBOFU MBOFU` YA SAMBA

753
0
SHARE
To the rescue: Fred scored the only goal of the game in Brazil's final warm-up before the World Cup

Fred flicked the ball home in the 58h minute to open the scoring at Morumbi Stadium

 Fred akichukua mpira katika dakika ya 58 na kufunga bao kwenye uwanja wa  Morumbi
Helpless: Branislav Ivanovic watches on but can't prevent the Brazilian forward from scoring

WAZEE wa Samba, Brazil,  jana usiku walibanwa mbavu na kuanza vibaya kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Serbia na kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakati huu zikisalia zimesalia siku tano tu kuanza fainali za kombe la dunia.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliofurika uwanjani waliwazomea wachezaji wa Brazil baada ya Fred kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 58.
Mchezo huo ulilalia kwa Serbia ambao walitengeneza nafasi nyingi hususani kipindi cha kwanza, lakini walikosa umakini.
Brazil walikoswa katika dakika ya 30 baada ya Aleksandar Mitrovic kupiga kichwa cha hatari na kutoka nje kidogo na  katika kipindi cha pili, Milos Jujic aliwakosa baada ya mpira wake kugonga mwamba.
 Hulk alifunga bao katika dakika ya 73 lakini lilikataliwa baada ya mwamuzi kuonesha alikuwa ameotea, lakini video za uwanjani zilionesha kuwa mwamuzi hayakuwa sahihi.
Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ya mwisho kwa wenyeji Brazil kabla ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia wiki ijayo katika uwanja wa Corinthians arena .
Brazil wanahodhi michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1950 na wapo kundi A na timu za Cameroon, Mexico na Croatia.

 Kikosi cha Brazil: Julio Cesar, Dani Alves (Maicon 71), Luiz, Thiago Silva, Marcelo (Maxwell 74), Gustavo, Paulinho (Fernandinho 64), Oscar (Willian 46), Hulk, Fred (Jo 75), Neymar.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Dante, Henrique, Ramires, Hernanes, Bernard, Victor.
Goli: Fred 58.
Kikosi cha Serbia: Stojkovic (Lukac 88), Basta (Tomovic 86), Ivanovic, Aleksandar Mitrovic, Kolarov, Dusko Tosic, Matic, Jojic, Tadic (Zoran Tosic 69), Petrovic (Mrdja 86), Markovic (Gudelj 81).
Wachezaji wa akiba: Pejcinovic, Djuricic, Stefan Mitrovic, Ljajic, Bisevac, Vulicevic, Lazovic, Brkic.

On the move: Neymar (right) fights for the ball with Serbia's Dusan Basta

Challenge: Brazilian forward Neymar is closed down by Chelsea's Ivanovic

 Huendi fundi: Mshambuliaji wa Brazil, Neymar akizuliwa na beki wa Chelsea, Ivanovic.
Partisan: Brazilian fans in Sao Paulo cheer their team's last game before the World Cup

 Mashabiki wa Brazil wakiishangilia timu yao katika mchezo wa mwisho wa kirafiki kuelekea kombe la dunia.
Passionate: The Sao Paulo crowd booed their team off at half-time after an uninspiring first period

 Walikosa uzalendo: Mashabiki wa The Sao Paulo waliwazomea wachezaji wao baaada ya kuonesha soka bovu kipindi kizima cha kwanza.
Message: Serbia players held up a banner as the two teams lined up before the game

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here