Home Kitaifa JULIAS KISARAWE KUVURUMISHIANA MAKONDE DHIDI YA MORO BEST JUN 7

JULIAS KISARAWE KUVURUMISHIANA MAKONDE DHIDI YA MORO BEST JUN 7

824
0
SHARE

julias kisarawe na morobest wakinyanyuliwa mikono juu kuashiria wamekubalika kuzipiga baada ya kupima na kwenda sawaBondia Julias kisarawe kesho anategemea kupanda ulingoni kuzipiga na Hassan kiwale “Morobest”  katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es salaa. Pambano hilo kali litakuwa  la raundi nane.

Akizungumza na vyombo vya habari , muandaaji wa pambano hilo, Sempai Gola na ofisa wa ngumi za kulipwa nchini,  Pembe Ndava kwa pamoja walisema maandalizi yote yamekamilika na mabondia wapo katika hali nzuri ukiondoa kasoro ndogo iliyojitokeza kwa Moro Best ambaye alitakiwa acheze na Fadhili Majia na sasa atacheza na Julias Thomas kisarawe ambaye ni mbadala mkali kwani bondia huyo hajapoteza mchezo katika michezo yake kumi na mbili aliyocheza.

Pambano hilo linategemewa kuanza jioni mida ya saa kumi na kutakuwepo na mapambano mengi mno ya utangulizi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here