Home Kitaifa ZAHORO PAZZI: LOGARUSIC HATAFIKA POPOTE KWENYE KAZI YAKE

ZAHORO PAZZI: LOGARUSIC HATAFIKA POPOTE KWENYE KAZI YAKE

1038
0
SHARE

NA Baraka Mbolembole
.Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba SC, Zahoro Pazzi amefunguka na kusema kuwa hatosaini klabu yoyote kama Simba itasitisha mkataba wake kama alivyoaagiza kocha, Z. Logarusic ambaye amemuweka mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Mtibwa Sugar, Azam FC, na Mtibwa Sugar pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania katika orodha ya wachezaji 13 ambao wanatakiwa kutemwa katika timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya nne ya ligi kuu.
Zahoro, alifanya mahojiano na mtandao huu siku ya jumatatu wiki hii amewahi kufanya majaribio nchini, Ujerumani mwishoni mwa mwaka 2012 kabla ya kupelekwa kwa mkopo JKT Ruvu ambako alicheza michezo isiyozidi saba na kuitwa timu ya Taifa, kisha akasajiliwa na Simba katikati ya mwaka uliopita na kocha, mzoefu nchini, Abdallah ‘ King’ Kibadeni. Alianza vizuri klabuni hapo kabla ya kupata majeraha na aliporejea uwanjani chini ya utawala wa kocha, Mcroatia, Logarusic hakuwa tena mchezaji ambaye awali wapenzi wa klabu ya Simba walimuona kama mchezaji sahihi wa kuziba nafasi ya Mrisho Ngassa ambaye alihamia kwa mahasimu wao Simba.
Wakati, juzi mchezaji wa kimataifa wa England, Frank Lampard  alitangaza kuwa ataondoka klabuni Chelsea baada ya kuitimikia kwa miaka 13 na kuweka rekodi ya ufunga ji wa muda wote klabuni hapo, Zahoro aliyeanza kucheza ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2008/ 09 baada ya kusajiliwa na klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro akitokea sekondari ya Makongo, tayari amepita klabu nne katika kipindi cha misimu mitano iliyopita katika ligi kuu ya Vodacom. Nilifanya mahojiano na kiungo huyo wa klabu ya Simba….

Zahoro, pole na msimu mgumu kwa upande wako na klabu pia.
ZAHORO; Asante, nimeshapoaaa.
SWALI; Kipi kimetokea katika uchezaji wako msimu uliopita?. ZAHORO; Sina la kujitetea, kuhusu kiwango changu msimu uliomalizika. Yanayotokea nikiwa timu kubwa sina la kuongea namuachia Mungu tu, sitaki kuonekana mchezaji nisiyekosa sababu wakati sipaswi kuwa hivyo. Sijisifii, ila ukweli ‘ najua sana kucheza mpira mpaka najitamani’

. SWALI; Tatizo ni nini, presha ya mashabiki au kuna kitu gani kinachokufanya ushindwe kufanya vizuri katika timu kubwa?
ZAHORO; Sihami kuwa presha ya mashabiki ndiyo sababu ya kufanya kwangu vibaya napokuwa ndani ya klabu kubwa. Mchezaji ukiwa na uwezo, suala la mashabiki kuwa wengi uwanjani linakufanya ufanye vizuri zaidi. Mfano, nilipokuwa, Azam si klabu yenye mashabiki wengi kama ilivyo kwa timu za Simba na Yanga, lakini hata pale soka lilikataa. Nilipoenda, JKT Ruvu nilicheza mechi chache tu uwezo wangu kila mtu aliuona, na nilirudi hadi katika timu ya Taifa. Sijui nini hutokea napokuwa timu kubwa. Sina la kusema kuhusu hilo, na hadi sasa sijapata majibu.

SWALI; Ulianza vizuri ukiwa chini ya makocha, ‘ King’ na Jamhuri Kiwelo. Ulipata majeraha lakini uliporejea uwanjani chini ya Mwalimu, Logarusic ulipata nafasi ila ukawa mchezaji wa hovyo uwanjani. Nini kilipelekea hali hiyo?
ZAHORO; Kocha ni mfano wa mzazi katika timu. Kama unapokuwa nyumbani na unapofanya makosa mzazi anakurekebisha, nafikiri katika timu jukumu hilo anakuwa nalo, Mwalimu. Kwa makosa ya ndani au nje ya uwanja yeye ndiye anaweza kumrudisha mchezaji katika njia sahihi. Ila, Loga hayupo hivyo.

SWALI; Ukipata nafasi ya kuzungumza naye kwa sasa, kipi unaweza kumwambia, na kitu gani kilikuwepo kati yako na Loga, kwani amezungumza mara kadhaa kuwa wewe si mchezaji mzuri?
ZAHORO; Sina cha kumwambia, ila nafikiri kwa mfumo wake wa kudili na mambo ya wachezaji hatofika mbali, si Simba tu, kokote kule atakapokuwa akifanyia kazi.

SWALI; Mtu anapofanya makosa hujutia makosa yake baadae, hivyo kama, Loga alifanya makosa yoyote unaweza kumwambia na mambo yakaenda vizuri.
ZAHORO; Mtu kama si mstarabu sidhani kama unaweza kumwmbia kitu akakuelewa. Loga, ni mtu mwenye dharau sana. Kuzungumza sana kuhusu yeye itakuwa kama natafuta sababu. Ila nimefanya kazi na Walimu wengi, King hajawahi kuniambia maneno ya kashfa hata siku moja. Nilipokosea aliniweka chini kunirekebisha. Loga ameshanitamkia maneno mengi ya kashfa ambayo sikuwahi kuambiwa na Salum Mayanga, Mecky Mexime, Marcio Maximo, Kim Poulsen. Kweli nilijiona sina thamani na kuwa mpweke ndani ya klabu. Nilijiona mimi ni mchezaji wa dharura iwapo, Amis Tambwe kaumia au anapoamuliwa ampumzishe. Iliniuma sana, ila ilinibidi nivumilie na kuwa mpole kwa sababu nipo kazi na ndani ya mkataba.

SWALI; Unawaambia nini mashabiki wa Simba?
ZAHORO; Bado ni mkataba na Simba, wao wanajua kuhusu uwezo wangu wa kucheza mpira, ila sitasaini timu yoyote kwa sasa kama mapendekezo yaliyotolewa na Loga ya kuondolewa katika kikosi yatafanyika.
ASANTE, wakati mwingine tena kiungo wa mpira.
ZAHORO; Asante pia, siku njema.
0714 08 43 08

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here