Home Makala WANACHAMA YANGA SC, BAADA YA UAMUZI NI UTII

WANACHAMA YANGA SC, BAADA YA UAMUZI NI UTII

860
0
SHARE

pmessNa Baraka Mbolembole
Narudia tena kusema; ‘ Mtu mkubwa ni Mwanafunzi’, na maana alisi ya neno falsafa ni ‘ Kutafuta busara, kupenda hekima’. Falsafa linatokana na maneno mawili ya Kiyunani; ‘ Philo’ lenye maana ya ‘ Upendo juu ya jambo fulani’ na ‘ sophia’ lenye maanaya ‘ busara’.
Nyakati za kale za kirumi, mwanafalsafa alikuwa ni mtu yeyote ambaye alionesha ubingwa wa kutafakari kwa busara na hekima masuala mbalimbali.
Katika nyakati za sasa neon falsafa hutumika kuelezea mtu anayefikiri kimantiki. Falsafa ni kutafuta –busara-hekima. Kila mmoja anaweza
kufikiri kwa namna yake na kusema lolote kuhusu uamuzi wa wanacha wa klabu ya Yanga kuachana na ajenda kuu ya marekebisho ya katiba ya klabu na kutumia muda mwingi katika mkutano mkuu kumuomba mwenyekiti aliyekuwa akitakiwa kumaliza muda wake wa uongozi, Yusuph Manji kuendelea kuongoza klabu hiyo.

Ilikuwa ni kitendo cha kishujaa kilichofanywa na wanachama hao kwa kuwa wameona kuwa wanahitaji uwepo wa Manji ili timu yao iendelee kuwa washindani katika soka la ndani. Pia, inawezekana wanachama hao wakawa wanahitaji kuona kiongozi huyo anabaki ili kuhakikisha wachezaji wao nyota hawaondoki klabuni hapo.

Mambo mawili katika demokrasi, ukiyakosa mambo hayo basi tambua hakuna demokrasia. Kwanza, kila mwanachama alipaswa kusema kwa uhuru, na maneno ya kila mtu yanapaswa kusikilizwa, hata kama mawazo yake hayapendwi kiasi gani. Kama mtu anapendwa kwa wema wake, au hapendwi kwa visa vyake, hayo yote si kitu. Kila mwanachama wa Yanga, lazima aweze kusema kwa uhuru. Watu wenye mawazo tofauti hata wakiwa wachache, ni lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao katika mkutanomkuu wa klabu bila hofu ya kusumbuliwa.
Mawazo yao yashindwe katika hoja za majadiliano. Majadiliano yenyewe yatakayoleta uamuzi lazima yawape watu nafasi ya kusema kwa uhuru, na hata baada ya kuamua jambo wanachama wawe na uhuru wa kuendelea kulizungumza jambo hilo. Wal wachache wenye mawazo tofauti lazima wafahamu kuwa kama wanayo mawazo yenye maana, na kama wakiyaeleza mawazo hayo vizuri. Wanaweza kubadili mawazo ya wale walio wengi.

Je, wanachama wa Yanga walikuwa na haja gani na mtu ambaye walimwambia hatishiki na pesa zake mara baada ya Azam FC kufanikisha
usajili wa wachezaji, Didier Kavumbagu na Frank Domayo , wachezaji hao walimaliza mikataba yao na Yanga na Domayo aligoma kusaini mkataba mpya, wakati Azam ilimuwahi Kavumbagu na kumpatia kitita kizuri cha pesa. Walisahau yote mara baada ya Manji kutoa ufafanuzi mzuri na kutoa ahadi kuwa ataisadia timu hiyo kufanya usajili mzuri kabla ya muda wake wa uongozi kumalizika. Wanachama walikuwa na jabza wakati ule lakini mbele yake wote walikuwa tayari kumuona akiendelea kuongoza klabu hiyo.

MIMI NI mmoja wa watu waliopendezwa na uamuzi wa pamoja wa wanachama wa klabu ya Yanga. Ukitazama kwa umakini utagundua kuwa klabu bado inamuhitaji, Manji ingawa yeye mwenyewe alishatamka kuwa inatosha. Inasemekana, Manji yupo mbioni kufuata nyayo za wafadhili na viongozi mbalimbali wa klabu za michezo ambao wamejikita katika mambo ya siasa. Ila, bado siamini kuwa mwaka mmoja aliouomba ili kujipima kiongozi klabuni hapo atautumia kujitangaza kiasasa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchini, mwishoni mwa mwaka ujao.

Ameongoza kwa miaka miwili, Yanga na Mama, Fatma Karume alimuomba kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa miaka nane zaidi, kitu ambacho, Manji alikikataa, na hata pale alipoombwa kuwania tena nafasi hiyo katika uchaguzi ambao kimsingi katiba inasema unapaswa kufanyika katikati ya mwaka huu bado mwenyekiti huyo alisema, hapana. Baada ya kuombwa sana na wanachama wa klabu, Manji akakubali huku akitoa mapendekezo yake. Kwanza, alitaka apewe muda wa mwaka mmoja zaidi kuendelea kuongoza.

Hapa alimaanisha uchaguzi mkuu usogezwe mbele kwa mwaka mmoja zaidi. Kikatiba wanachama wa klabu wanayo haki ya kusogeza mbele mkutano mkuu wa uchaguzi kama maamuzi ya pamoja yatafikiwa na kukubaliwa. ‘ Maamuzi bab-kubwa’ yakafikiwa baada ya wanachama kupiga kura za ‘ NDIYO’ au ‘ HAPANA’, hapo uamuzi uliofikiwa ni kuendelea kumuongezea muda wa uongozi, Manji naye akakubali. Hiyo ndiyo misingi ya demokrasia popote pale na Yanga wameruka ‘ kihunzi’ walichojikwaa mahasimu wao.

Pia, Manji ameomba utulivu klabuni kwa muda wote atakao kuwa madarakani, hapa alikuwa akifikisha ujumbe kwa Baraza la Wazee la
klabu kuachana na malumbano yasiyo na tija. Ni kweli, baraza hilo linapaswa kuheshimu katiba na taratibu za klabu popote pale wanapokuwa wakizungumza kuhusu, Yanga. Mzee, Akilimali na wenzake wanaweza kutumia busara na hekima yao kumshahuri, mwenyekiti kwa njia za kistaarabu, huku wakitambua mawazo yao yanaweza kukubaliwa na kufuatwa kama yatakuwa ni mazuri, na yatawekwa kando ikiwa hayatakuwa na manufaa.

Watumie nafasi yao vizuri na si kukimbilia katika vyombo vya habari na kuzungumza kuhusu mambo muhimu ya klabu, tena wakiwashutumu waziwazi wachezaji pale wanapofanya makosa ya kimchezo uwanjani. Miaka mitatu itamtosha kujua anaweza kuifanyia nini Yanga kama atakuwa madarakani kwa miaka mine au nane ambayo ameombwa na baadhi ya wanachama. Ndani ya uwanja Yanga ni timu iliyokaa pamoja kwa miaka mingi hivyo itakuwa kosa kuona timu ikivurugika kwa kukosa uongozi makini.
Mtazamo wa Manji kuhusu timu ndani ya uwanmja ni kufanya vizuri katika michezo ya Afrika, na kwa timu iliyopo sasa na namna kiongozi huyo anavyodili na wachezaji kama Athumani Iddi, Nadir Haroub, na wengine ambao wakati Fulani wanasukumwa nje ya timu na wanachama wenye jabza ni kielelezo tosha kuwa wanachama wa Yanga wamefanya maamuzi sahihi. Sasa ni wakati wa kuyatii maamuzi hayo. Manji ana miaka miwili tu tangu alioanza kujifunza kuhusu mambo ya uongozi wa soka, alikuwa na sababu za msingi kuomba mwaka mmoja zaidi ili ajipime.

Kuongoza Yanga kwa siku moja ni kazi kubwa, ila ilikuwa ni ushujaa mkubwa kwake kuona akililiwa kuendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo. Naamini ataendelea kujifunza zaidi na mwaka mmoja huo hautakuwa wa nia ya kujitangaza kisiasa zaidi ya kuhakikisha Yanga inatinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika. Uliona ukuta wa jana wa Taifa Stars? Wachezaji wanne kati ya watano wanatoka Yanga na pengine wasingekuwepo kikosini endapo wasingekuwa chini ya mwenyekiti mwenye upendo na busara. Yanga imevuka salama majira haya ya usajili sasa ni kuimarisha kikosi, uamuzi uliofikiwa uwe na utii.

0714 08 43 08

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here