Home Dauda TV Bosnia and Herzegovina-KUTOKA KWENYE MAPIGANO MAKALI HADI KUWAPA RAIA FARAJA….

Bosnia and Herzegovina-KUTOKA KWENYE MAPIGANO MAKALI HADI KUWAPA RAIA FARAJA….

641
0
SHARE

Jina la mshambuliaji wa klabu ya VFB Stuttgart ya nchini Ujerumani, Vedad Ibiševic mwaka uliopita liliingia kwenye akili za watu wa taifa dogo la Bosnia na Herzegovina, baada ya staa huyo kufunga bao muhimu lililoipeleka nchi hiyo kwenye fainali zake za kwanza za kombe la dunia..

Taifa dogo kabisa barani Ulaya likiwa na idadi ndogo ya wananchi, ambao si zaidi ya milioni nne, wanafuzu kwa fainali za mwaka huu za kombe la dunia, mara ya pili katika historia, tangia England ilipofanya hivyo, tena kwenye fainali zilizofanyika nchini Brazil kama mwaka huu, England ilifanya hivyo mwaka 1950, ikiwa taifa lenye watu wachache pia.

Taifa hili dogo lilipangwa na nchi kama Greece, Slovakia, Lithuania, Latvia na Liechtenstein kwenye kundi la G, ambapo kampeni yake ilianza kwa kuipa kisago cha mbwa mwizi Liechctenstein cha mabao manane kwa moja, kisha ikaipiga Latvua manne kwa moja nyumbani mjini Zenica, kabla ya suluhu tasa dhidi ya mabingwa wa zamani wa Ulaya Ugiriki, tena ugenini mjini Piraeus, na kuipigilia Latvia matatu kwa sifuri.

Pamoja na kumkosa mkali wake Miralem Pjanić aliyekuwa majeruhi kwenye mechi ngumu ya kufuzu dhidi ya Ugiriki mnamo March 22’2013, bado walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja, ambapo mkali wake mwingine Edin Džeko alifunga mara mbili, na baadae kuiburuza tena Latvia matano kwa sifuri.

Bado kipigo cha bao moja kwa sifuri walichokipata toka Slovakia mnamo September 2013 nyumbani mjini Zenica hakikuwaondoa kwenye kampeni zao za kufuzu, pamoja na kuwa sawa kwa pointi na mabaharia wa Ugiriki, na wakageuza tena matokeo ya kufungwa na Slovakia nyumbani, baada ya kushinda mbili moja ugenini mjini Zilina.

Bosnia na Herzegovina,chini ya meneja wake Safet Sušić, walijihakikishia kufuzu kwa fainali hizo baada ya ushindi wa moja sifuri ugenini dhidi ya Liechtenstein na dhidi ya Lithuania mjjini Kaunas on 15 October 2013 na sasa wakawa juu ya kundi la G, mbele ya Ugiriki, huku mkali wake Edin Dzeko akiwa mfungaji bora wa pili kwenye michuano ya kufuzu kwa kanda ya bara la Ulaya, nyuma ya Robin van Persie akifunga mabao kumi.

Kumbuka kwamba, taifa hili, ni sehemu ya lililokuwa taifa kubwa la iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia, na baadhi ya nyota wake walikuwa pamoja hadi mnamo mwaka 1992.. lakini nani asiyemkumbuka nyota kiraka, hodari na mvumilivu Hassan Salihadmizic aliyekuwa staa wa Juventus???

The Team is governed by the Football Federation of Bosnia and Herzegovina (N/FSBiH). Until 1992, Bosnian-Herzegovinian players were part of the SFR Yugoslavia national football team.

Nyota bora wa Bosnia na Herzegovina walicheza kwenye madaraja ya kwanza, ya pili na tatu, ndani ya iliyokuwa Yugoslavia, ambao ni kama Vahid Halilhodžić, Safet Sušić, Josip Katalinski, Faruk Hadžibegić, Ivica Osim, Asim Ferhatović, Blaž Slišković, Mehmed Baždarević, Dušan Bajević ambao waliiwakilisha Yugoslavia, kimataifa..

Muda mfupi, baada ya uhuru wa Bosnia na Herzegovina toka iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia, nyota walioteuliwa timu ya taifa walicheza chini ya jina, “Bosnia-Herzegovina Humanitarian Stars” mchezo ulibeba jina la Upendo, tena nje ya nyumbani, dhidi ya tvilabu ya K.R.C. Genk ya Ubelgiji na FC Kaiserslautern ya Ujerumani, mnamo mwaka 1993.

Mamlaka kuu za mchezo wa soka duniani Fifa, zilianza kuitambua michezo ya kirafiki ya Bosnia na Herzegovina siku tisa baada ya yale makubaliano ya Amani ya Dayton, yalioashiria mwisho wa vita ya Bosnia, iliyopigwa mjini Tirana dhidi ya Albania, mnamo  14 December 1995.

Timu ya taifa ya Bosnia na Herzegovina haikutakiwa kucheza michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 1994, hadi ilipokwa mwanachama wa Fifa mnamo July 1996 lakini pia UEFA iliwapa uwanachama mwaka 1998 mjini Dublin na tena ikikosa kushiriki michuano ya kuwania kufuzu kwa Euro 1996 nchini England.

Mnamo April 25’ 2000, Bosnia na Herzegovina ilicheza mchezo mwingine wa hisani, dhidi ya timu ya wanandinga wa kikosi cha kwanza cha kombe la dunia, ukiwa ni mahsusi kwa yatima wa nchi hiyo kwenye uwanja wa Kosevo mjini Sarajevo, ambapo walilala bao moja kwa sifuri, la Robert Baggio wa Italia la mkwaju wa penati, mchezo ambapo nyota kama Carlos Dunga wa Brazil na Ali Daei wa Iran walicheza. also made appearances for the World XI.

Kwenye michuano ya kufuzu kwa Euro 2004 nchini Ureno, ni bao moja tu kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Denmark, lilitosha kuiweka pembeni timu hiyo, isifuzu..

Bado pia taifa hili lina kumbukumbu ya kufungiwa na Fifa mnamo mwaka 2011..

Kizazi cha sasa cha akina  Senijad Ibričić, Boris Pandža, Edin Džeko, Vedad Ibišević na Sejad Salihović,aliyecheza kwenye michuani ya vijana ya Uefa ya mwaka 2007, wapo tayari kuonyesha maajabu katika mashindano yao makubwa ya kwanza..

IMEANDALIWA: IBRAHIM MASOUD ‘MAESTRO’

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here