Home Makala KUTOKA UCHEZAJI HADI UFUNDISHAJI JUMA KASEJA ANAWEZA KUWA KOCHA MZURI

KUTOKA UCHEZAJI HADI UFUNDISHAJI JUMA KASEJA ANAWEZA KUWA KOCHA MZURI

1512
0
SHARE

kasejaNa Baraka Mbolembole
Golikipa wa zamani wa timu ya soka ya Simba, Juma Kaseja, 29 katikati ya mwanzoni mwa wiki hii alikuwa mmoja wa watu watatu kati ya 34 waliohitimu mafunzo ya ukocha daraja A. Kaseja ambaye anaichezea timu ya Yanga kwa sasa, alianza kucheza ligi kuu Tanzania Bara, mwaka 2001 katika timu ya Moro United akiwa na miaka 17, amecheza katika klabu tatu tofauti nchini katika muda wa miaka 13 sasa. Ni mafanikio ambaye yatamfanya kuwa tayari kwa kazi ya ukocha miaka ya mbele. Mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo, Kaseja alisema bado ataendelea kucheza soka huku akitumia kozi hiyo ya mafunzo ya ukocha kujihimarisha zaidi kiuchezaji kwa kuwa ameweza kufahamu mambo mengi ya kiufundi ambayo awali hakuwa akiyafahamu vizuri au kuyajua kabisa.
Kuna wachezaji wachache sana ambao wamefikia mafanikio yake ya kiuchezaji. Akiwa mshindi wa mataji saba ya ligi kuu Tanzania Bara, huku akiwa na tuzo nyingi binafsi, Kaseja anafuata mkumbo wa wachezaji wengi wa soka barani Ulaya ambao waliingia katika mafunzo ya ukocha wakiwa badowachezaji. Wiki hii klabu ya FC Barcelona, ilitangaza kumpatia majukumu ya ukocha mchezaji wao wa zamani, Luis Enlique, Manchester United itaongozwa na mchezaji wake wa zamani, Ryan Giggs ambaye ameamua kustaafu kucheza soka la ushindani, Claude Makelele ameachia kazi ya usaidizi chini ya Laurent Blanc katika klabu ya PSG na kuanzia msimu ujao atakuwa kocha wa timu ya Bastia ambayo pia inacheza katika ligi kuu ya Ufaransa, Lieague 1.

juma-kasejaWilly Sagnol mlinzi wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich anataraji kuwa kocha mkuu wa mabingwa wa zamani wa Liegue 1, klabu ya Bordeaux. Si hao tu, tumeshaona mafanikio ya makocha kama, Pep Guardiola, Carlo Ancelotti, Gustavo Poyet, Diego Simeone na wengineo ambao waliingia katika kazi ya ukocha na kufanikiwa muda mfupi baada ya kustaafu soka. Ukitoa, Kaseja, kwa upande wa Tanzania wapo wachezaji wengi wa zamani ambao walijitumbukiza katika kazi ya ukocha lakini hakuna ambaye ameweza kupata mafanikio yanayoonekana. Si kwamba hawana uwezo, hapana, bado watawala wa soka Kwa nini wachezaji wa zamani wa Tanzania wanashindwa kufikia mafanikio hayo?
Mtazame kocha Juma Mwambusi, Mwalimu huyo amekuwa akionesha uwezo mkubwa wa ufundishaji katika miaka ya karibuni . Mwaka 2008, aliisaidia klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu Tanzania Bara, na msimu uliomalizika aliweza kuisaidia timu iliyokuwa ikicheza ligi kuu kwa mara ya kwanza kumaliza katika nafasi ya tatu. Mwambusi ambaye aliwahi kuifundisha timu ya Polisi Dodoma na kushuka daraja chini yake, aliipandisha daraja Mbeya City na kufanya mambo makubwa ila bado hakuna uwezekano way eye kufundisha klabu kubwa za Tanzania kwa kuwa timu hizo zimewekeza mawazo yao kwa Walimu wa kigeni.
Kwa sasa Tanzania imekuwa ikiweka mkakati wa kuinua soka la ndani, ila mkakati huo ni lazima uendane na maboresho ya miondo mbinu, viwanja, timu za watoto na kuwaendeleza makocha wazawa kwa kuwapatia kozi zaidi ambazo zitawaongezea ujuzi wa ufundishaji. Si kila mchezaji mahiri anaweza kuwa kocha bora ila ukitoa , makocha kama Charles Boniface Mkwasa, na Abdallah Kibadeni, makocha wengine wakiongozwa na Jamhuri Kiwelo na Fred Minziro japokuwa walicheza kwa mafanikio katika klabu za Simba na Yanga, na kuonesha uwezo wao wa ufundishaji wakiwa katika klabu ndogo wameishia kuwa makocha wasaidizi na si rahisi kwao kuwa makocha wakuuu katika klabu hizo. Kwa nini?

JUMA_KASEJA[1]Mfumo wa ufanyaji kazi kwa mazoea kutoka kwa viongozi wengi wa soka nchini umepelekea wachezaji wengi wa zamani kushindwa kupata mafanikio katika kazi ya ukocha . Wapo wanaosema kuwa mapenzi ya u-Simba na u-Yanga yamefanya wapenzi wengi kukosa imani na makocha wazawa kupewa kazi hiyo, Simba ama Yanga na badala yake wamekuwa wakirubuniwa kutoka timu ndogo kila wanapofanya vizuri na kupewa kazi ya usaidizi katika timu hizo wanazozifahamu vyema. Hili ni kosa, ni lazima tuwapromoti makocha wetu wazawa ili siku moja waweze kusaidia mpira wa Tanzania kwa kuzalisha wachezaji wengi vijana.
Mecky Mexime ameichezea Mtibwa kwa maisha yake yote ya soka la ushindani, na sasa akiwa na miaka miwili katika kazi ya ukocha wa timu hiyo, Mecky anatakiwa kupandisha kiwango chake cha ufundishaji ili kujiweka katika orodha ya makocha ambao Tanzania inaspaswa kujivunia. Mecky angweza kuwa kama Gary Neville ambaye mara baada ya kustaafu soka la ushindani, Roy Hodgson alimchukua Neville na kumfanya msaidizi wake katika timu ya England jambo ambalo kwetu sisi si rahisi kutokea kwa kuwa ni wachezaji wachache ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kweli za kuwa makocha bora.
Kwa nini, Suleiman Matola anakuwa kocha msaidizi katika timu ya Simba hadi hivi leo?. Matola amechezea Simba kwa mafanikio makubwa, zaidi tangu alipojiingiza katika kazi ya ukocha ameonesha kitu kikubwa anacho. Matola ni mshindi kiuchezaji na kiufundishaji. Ameshinda mataji kadhaa ya Uhai Cup akiwa kocha wa kikosi cha pili, aliwahi kushinda ubingwa wa kombe la Taifa Cup akiwa kocha wa Mkoa wa Singida na zaidi ndiye ambaye amewezesha timu ya Simba kuwa na vijana bora ambao kwa miaka miwili ya ukata klabuni hapo chipukizi hao wameweza kuziba virika Simba. Huyu ana uwezo mkubwa wa kiufundishaji lakini mbona bado makocha wetu wazawa hawapandishwi na kuwa makocha wakuu katika klabu kubwa?
UKitoa udhaifu wetu wa kuhitaji mambo makubwa na sifa , makocha wenyewe wanaweza kujifunza zaidi na kupandisha viwango vyao ambavyo vinaweza kuzivutia timu za jje ya nchi na wakaenda huko kupata uzoefu wa kiufundishaji. Mbona kina, Tom Olaba , Sam Timbe, James Siang’a, Moses Basena na wengine wanatoka nchi za Kenya na Uganda na kuja Tanzania kuzifundisha timu zetu kubwa? Hongera, Juma Kaseja kwa kujiandalia mazingira ya kazi mpya siku za mbeleni. Kutoka uchezaji, hadi ufundishaji, Juma Kaseja anaweza kuwa kocha mzuri katika miaka ijayo kama tutajifunza kutokana na makosa yetu.
0713 08 43 08

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here