Home Dauda TV MDAU WA RIADHA WILHELM GIDABUDAY AIOMBA SERIKALI KUWAFUKUZA VIONGOZI WA RT……

MDAU WA RIADHA WILHELM GIDABUDAY AIOMBA SERIKALI KUWAFUKUZA VIONGOZI WA RT……

729
0
SHARE

Two years Anniversary of Illegal Elections held in Morogoro May 20th, 2012 under supervision of Leonard Thadeo and National Sports Council of Tanzania; ‘It’s a shameful act’

(1)May 20th, 2012 RT walifanya uchaguzi kwa MOU ambapo walisaini kwamba baada ya siku tisini viongozi watakuwa na katiba mpya ama sivyo watakuwa wamevunja mapatano, August 20th, 2012 siku tisini zilitimia.

 

(2)                       Leo tarehe 20th 2014 ni miaka miwili kamili imepita bila katiba mpya wala mafanikio yoyote katika mchezo wa riadha zaidi ya aibu kwa taifa letu.

 

(3)                      Inaelezwa kwamba mwaka mzima umetimia bila kikao cha kamati ya utendaji kufanyika kama ilivyo sheria, kanuni na taratibu za lazima za BMT.

 

(4)                    Leo hii RT imeburuzwa mahakamani (TEMEKE) kwa kudaiwa zaidi ya TSH: 20,000,000 kwa sababu ya uzembe wa viongozi wa taasisi hiyo isiyo na katiba inayotambulika.

 

(5)                        Mapema mwezi huu timu za kwenda kambini nje ya nchi zilichaguliwa mezani badala ya kuchaguliwa viwanjani kwa vigezo vya kushindanishwa ili walio bora wapelekwe.

 

(6)                    Mbaya zaidi timu iliyokwenda New Zealand imeripotiwa kubadilishwa majina kinyemela na kuonekana waliotajwa kuondoka (Mwa.Samwel Tupa na mwanariadha Atson Mbuga) wapo Arusha na Tanga. Je nani kaneda? Je posho yao kala nani?

(7)                     Mheshimiwa waziri hata kwa macho tu hayo yanayofanywa na viongozi wa RT huyaoni, pia waheshimiwa wa BMT kimya chenu kinampatia nani tija?

 

(8)                    Mkurugenzi wa Michezo (LEONARD THADEO) ndiye mvunjaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu kwani yeye ndiye anayewakingia kifua viongozi haramu wa RT pia ni yeye alisimamia uchaguzi wa MOU.

 

(9)                    Baada ya hayo yote kutokea; Je Anthony Mtaka na nduguye wa ukoo Suleiman Nyambui bado wana uadilifu usiotiliwa shaka kuendelea kuongoza RT?

 

(10)               Kwa mtindo huu wa kupenyeza wasiohusika katika safari haiwezi kutumiwa na vikundi hatari kama Al Shaabab na wauza unga?

 

Arranged and written by:

Wilhelm Francis Gidabuday.

0786778421 / 0752778422.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here