Home Makala LUIS ENIRIQUE, AMERUDI NYUMBANI KURUDISHA MAKALI YA BARCELONA

LUIS ENIRIQUE, AMERUDI NYUMBANI KURUDISHA MAKALI YA BARCELONA

859
0
SHARE

article-2633039-1E03B23E00000578-853_634x370
Na Baraka Mbolembole
Baada ya kumaliza msimu pasipo kutwaa ubingwa wowote, kocha, Martino aliamua kuachia kazi yake mara baada ya kikosi chake kulazimishwa sare na Atletico Madrid, siku ya jumamosi iliyopita. Baada ya kuisaidia, Barcelona kutwaa taji la Super Coppa kwa sheria ya goli la ugenini dhidi ya Atletico, kocha huyo raia wa Argentina aliifikisha, Blaugrana hatua ya fainali ya kombe la Mfalme, ambayo walipoteza mbele ya mahasimu wao Real Madrid, pia aliisaidia kufika nusu fainali ya michuano ya mabingwa Ulaya, wakitolewa na Atletico, na kumaliza nafasi ya pili katika ligi kuu, La Liga. Martino ameondoka huku timu hiyo ikiwa imepoteza makali yake ya kawaida ndani ya uwanja.
Aliyekuwa kocha wa timu ya Celta Vigo, Luis Enrique Martinez Garcia amepewa kazi hiyo ya kuisuka upya Barcelona ambayo imeshindwa kutwaa taji lolote msimu huu baada ya misimu mitano ya mataji mfululizo. Enlique, mchezaji wa zamani wa timu za Real Madrid na Barca, alianza kazi ya ukocha mwaka 2008, katika timu ya Barcelona B ( timu ya pili ya FC Barcelona), akichukua nafasi ya Pep Guardiola ambaye alikuwa amepandishwa katika kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Frank Rijkaard, katikati ya mwaka huo.
Pep, alifanikiwa kwa kiwango kikubwa katika timu hiyo, akishinda mataji 16 katika misimu minne klabuni, Camp Nou. Enlique aliisaidia, Barcelona B kupanda katika ligi daraja la pili baada ya miaka 11. Aliifundisha timu hiyo hadi 2011, na ilipofika, juni 8, akasaini mkataba wa miaka miwili wa kuifunza timu ya AS Roma ya Italia. Kipenzi huyo wa mashabiki wa Barca, Enlique aliondoka Italia mwaka mmoja baada ya kushindwa kuisaidia, Roma kupata nafasi ya kucheza michuano yoyote ya Ulaya.
Aliamua kurudi, Hispania, na juni 8, 2013 alisaini kujiunga na Celta Vigo ambayo ameisaidia kumaliza katika nafasi ya tisa katika msimu uliomalizika kwa Atletico Madrid kutwaa taji hilo la La Liga…. Wakati wa uchezaji wake, Enlique alishinda taji moja la La Liga katika misimu yake mitano, Real Madrid na alishinda mataji mengine mawili katika klabu ya Barcelona ambayo aliichezea kwa miaka nane, 1996-2004 alipostaafu soka la ushindani akiwa na miaka 34.
Alicheza michezo 400 na kufunga magoli 104 akiwa na klabu hizo kubwa za Hispania, kiungo huyo wa mashambulizi wa zamani aliiwakilisha timu ya Taifa ya Hispania katika fainali tatu tofauti za kombe la dunia, 1994, 1998, na 2002, alifunga magoli 12 katika michezo 62 ya La Roja.
ATAPITA NJIA GANI?
Siku ya kwanza ya Pep katika mazoezi ya Barca alimuita pembeni kiungo, Xavi Hernandez na kumueleza maneno machache ila yalikuwa muhimu sana. Pep, ni ‘ bonge la kocha wa kisasa’, unajua alimwambia nini, Xavi?. Guardiola alirithi iliyokuwa imetwaa mataji mawili ya La Liga katika kipindi cha miaka minne chini ya mtangulizi wake, Rijkaard, taji moja la ulaya, lakini haikuwa na ubingwa wowote kwa miaka miwili ya mwisho. Pep, alitangaza mapema kutowahitaji nyota watatu ambao, Rijkaard aliwafanya muhili wa timu ndani ya uwanja, Ronaldinho Gaucho, Deco De Souza na Samuel Eto’o.
Wachezaji hao watatu walitua, Camp Nou kati ya miaka ya 2003 na 2004, na kuifanya timu hiyo kushinda ubingwa wa kwanza wa La Liga baada ya kuusotea tangu mwaka 1999, na walifanikiwa kushinda taji la kwanza la Ulaya, mwaka 2006 tangu, mwaka 1992. Gaucho akiwa na tuzo mbili za mwanasoka bora wa dunia, alikuwa ameshuka kiwango kwa kuendekeza mambo ya nje ya uwanja, alikuwa mtu wa kujirusha kila mara, Deco, alikuwa katika kipindi cha majeraha, ila naye alikuwa na tabia ya kumuendesha kocha wake, Eto’o alikuwa staa wa timu na kundi la nyota hao watatu halikuonesha tamaa ya kusaka mataji zaidi kwa kuwa tayari walikuwa ni washindi na wachezaji muhimu waliofanikiwa kurudisha mataji, Camp Nou. Miaka miwili ya mwisho ya Rijkaard ilikuwa ni mibaya, kwani wachezaji wake muhimu hawakuwa wakimuheshimu kama mwanzo.
Pep, alitaka kitu tofauti!. Alitaka kuitengeneza upya Barcelona, na kitu muhimu cha kwanza ni kutengeneza muhimili wa kikosi chake. Mpango wake aliuelekeza, La Masia- Shule ya vipaji vya soka ya klabu hiyo. Alimwambia, Xavi kuwa anataka kuona akimsaidia, Andres Inesta na kuimarisha mahusiano yao ya kiuchezaji kwa kuwa alipanga kuwatumia wao zaidi kama muhimili wa timu. ‘ Unamuona kijana yule ( akimuonesha, Iniesta) naomba umpatie ushirikiano’, kisha akampandisha kiungo Sergio Busquets aliyekuwa na miaka 19 kutoka timu B, na kutengeneza safu imara ya kiungo.
Hakuishia hapo, alimsajili mlinzi, Gerlad Pique kutoka, Manchester United ili kusaidiana na Carles Puyol, Rafaer Marquez, Eric Abidal, na Edmilson. Barca ikawa imara tena, ikaanza msimu kwa kutandaza soka safi, timu ilikuwa ngumu kufungika, ilikuwa ikitawala nafasi ya kiungo katika kila mchezo, ikawa inafunga magoli ya kutosha. Leonel Messi alikabidhiwa majukumu aliyokuwa nayo, Gaucho, zaidi, Muargentina huyo alikuwa hatari katika ufungaji. Akishirikiana na Eto’o aliyekosa timu ya kumnunua, na Thiery Henrry, Pep alikuwa na mastraika watatu-wafungaji, wakapachikwa jina la ‘ Utatu Mtakatifu’ na waliweka rekodi ya kufunga magoli 97 kwa pamoja katika msimu wa 2008/09, ambao walitwaa vikombe vitatu.
Pep, alishinda, Copa del Rey, La Liga na Ligi ya mabingwa huku timu ikicheza kandanda la kuvutia. Mpango wa kuwatumia vijana wa La Masia ulikuwa na mafanikio makubwa huku wachezaji, Victor Valdes, Puyol, Pique, Busquets, Iniesta, Xavi, Messi, na Pedro Rodriguez ambaye alipandishwa kutoka kikosi cha pili wakifanya vizuri kiuchezaji. Pep, alifanikiwa, Barcelona, ila ni kwanini aliamua kung’atuka?
KUWAONDOA BAADHI YA WACHEZAJI NA KUWALETA WALIO SAHIHI
Pep alimsajili mlinzi wa kulia, Dan Alves mara baada ya kupewa kazi hiyo/ Dan aliongeza kitu kikubwa katika timu hiyo na akatokea kuwa mmoja wa wachezaji hatari zaidi wa ulinzi kuwahi kutokea katika La Liga, ila ni miongoni mwa wachezaji wane ambao walisababisha kuondoka kwa Pep. Kivipi? Mara baada ya Barca kuambulia taji moja katika msimu wa 2011/ 12, Pep alitaka kufanya mabadiliko makubwa katika timu. Alimwambia aliyekuwa rais wa timu hiyo Sandro Rossel kuwa atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuifunza timu hiyo kama atakubali kufanya mabadiloko.
Kwanza alihitaji kuona wachezaji, Alves, Cecs Fabregas, David Villa na Pique wakiuzwa na kusajiliwa nyota wengine. Kwa madai yake aliona kuwa Alves ametosheka na mafanikio aliyokuwa ameshayapata katika uchezaji wake hivyo hakuwa na hamu ya kujituma zaidi kwa maslai ya timu. Alitaka kuona Pique akiuzwa kwa kuwa mlinzi huyo alikuwa akithamini zaidi maisha yake ya nje ya uwanja kuliko kuisaidia timu. Akaendelea kwa kusema kuwa, Fabregas alimnunu kwa pesa nyingi ili kuja kuongeza nguvu katika timu lakini nyota huyo wa zamani wa Arsenal ameshindwa kuisaidia timu hiyo wakati ilipokuwa ikimuhitaji kufanya hivyo hasa wakati viungo, Xavi na Iniesta walipokuwa na majeraha, na akamwamwimbia, Sandro kuwa atahitaji mshambuliaji makini zaidi kuliko Villa kwa kuwa nyota huyo wa Hispania alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara hasa wakati timu ikihitaji huduma yake.
Sandro, akamwambia kuwa nyota hao wote wane ‘ hawagusiki’ na kama watafanya hivyo watawatibua mashaniki wa klabu. Pep akaamua kutosaini mkataba mpya na timu hiyo akapewa marehemu, Tito Vilanova ambaye awali alikuwa msaidizi wa Pep kwa misimu mine. Tito ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi aliisadia Barca kutwaa ubingwa wa La Liga, lakini vipigo vikubwa katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya Ulaya kutoka kwa FC Bayern Munich vilitosha kuthibitisha maneno ya Pep kuhusu nyota hao. Mara baada ya kuondoka kwa, Vilanova, Barca ilimpatua timu Martino ambaye ameshindwa kushinda taji lolote nay eye mwenyewe akaamua kukaa kando.
Enrique anatakiwa kusajili wachezaji wa idara ya kiungo na wale wa ulinzi wa kati na pembeni, huku akiwauza nyota kama Fabregas, Alexs Sanchez, Javier Mascherano, na kutafuta mlinzi mwenye sifa za Puyol ili kusaidia na Pique ambaye msimu uliopita alionekana kutuliza akili yake uwanjani na kucheza kwa maslai ya timu. Barca itarejea tena msimu ujao chini ya mchezaji wao wa zamani ambaye alicheza kwa miaka mitano, Santiago Bernabeu lakini bado akawa kipenzi cha Blaugrana alipotua kama mchezaji huru, Camp Nou wakati wa usajili wa majira ya kiangazi mwaka 1996. Ni mshindi wa taji la UEFA hivyo bila shaka huyu ni mtu sahihi ambaye atairudisha FC Barcelona katika makali yake msimu ujao. Amerejea nyumbani mahali alipomalizia soka lake na kujifunza kuhusu taaluma ya ukocha.
0714 08 43 08

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here