Home Kitaifa MBEYA CITY FC YAENDELEA KUJIWINDA NA CECAFA NILE BASIN CUP JIJINI DAR

MBEYA CITY FC YAENDELEA KUJIWINDA NA CECAFA NILE BASIN CUP JIJINI DAR

743
0
SHARE

IMG_1150Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City fc bado ipo jijini Dar es salaam kujiandaa na safari ya kwenda Sudan kushiriki michuano mipya ya CECAFA Nile Basin inayotarajia kuanza mei 22 mpaka juni 4 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi ameuambia mtandao huu kuwa asubuhi hii wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu tupo hapa Karume. Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu. Na mambo yakikaa sawa muda wowote tutaanza safari ya kwenda Sudan”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji wote wapo katika morali kubwa na wanahamu kubwa ya kwenda kushiriki michuano hii mikubwa.
“Wachezaji wetu siku zote wanapenda kucheza. Hii ni nafsi nyingine nzuri ya kupata uzoefu wa michuano ya kimataifa. Najua itakuwa changamoto kwetu, lakini tutapambana kwa kila mechi”.
“Sisi bado ni wachanga katika soka. Michuano kama hii ni msingi mzuri kwetu”
“ Tutaitumia vyema nafasi hii kuhakikisha tunafanya vizuri, tumekuwa tukitumia muda mwingi kuwapa mbinu za kimpira wachezaji wetu”. Aliongeza Mwalwisyi.
Mwalwisyi aliwaomba mashabiki wao na watanzania wote kuwaombea mafanikio katika mashindano hayo kwasababu kufanya vizuri itakuwa sifa kwa taifa zima.
Mbeya City fc waliopo kundi B wataanza kampeni zao mei 23 kwa kukabiliana na El Merreikh Al Fasher .

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here