Home Makala TAIFA STARS VS THE WARRIOS; KNOWLEDGE MUSONA NI MTU WA KUCHUNGWA SANA

TAIFA STARS VS THE WARRIOS; KNOWLEDGE MUSONA NI MTU WA KUCHUNGWA SANA

865
0
SHARE

DSC_4490Na Baraka Mbolembole

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itawasili, jijini, Dar es Salaam, siku ya kesho ikitokea katika kambi ya wiki mbili, jijini, Mbeya. Stars ilicheza na timu ya Taifa ya Malawi, wiki iliyopita katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki na kulazimishwa suluhu-tasa katika uwanja wa Sokoine, Mbeya. Kikosi cha kocha, Martin Nooij kitapambana na timu ya Taifa ya Zimbabwe, The Warrios, siku ya jumapili ijayo katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, mwakani, nchini, Morocco.
Zimbabwe ni timu inayoundwa na wachezaji wengi vijana wanaocheza ndani na nje ya nchi yao. Walikuwepo katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN 2014, na walifika mbali katika michuano hiyo iliyofanyika, Afrika Kusini mwanzoni kabisa mwa mwaka. Ikiwa na golikipa mzoefu, Washington Arubi, 28 kikosi hicho cha kocha, mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Ian Kuziva Gorowa, The Warrios wamekuwa na timu imara katika idara ya ulinzi.

Lakini, bado washambuliaji wa Stars, Mrisho Ngassa na John Bocco, wanaweza kutumia uzoefu wao kuisaidia Tanzania kupata ushindi. Kocha, Ian, amekuwa akipendelea kuichezesha timu yake katika mfumo wa 4-4-2, kwa kuwapanga walinzi, Hardlife Zvirekwi, 27, Milton Naub, 26, huku mchezaji mwenyewe umri mkubwa katika safu hiyo ya ulinzi, Carlington

Nyadombo, 28 anayekipiga katika timu ya Amazulu ya Afrika Kusini, na Gift Belo anayechezea klabu ya Platinum pia ya Afrika wakikamilisha safu ya ulinzi ya Zimbabwe. Ukitazama, utaona wachezaji watatu kati ya watano wa safu hiyo ya nyuma wanacheza katika ligi kuu ya Afrika Kusini.

Nafahamu, kuwa hicho si kigezo kikubwa cha Stars kushindwa kufunga magoli. Stars inaweza kunufaika kwa kucheza nyumbani, ila itakuwa ni hatari kubwa kama timu itakwenda, Harare ikiwa na ushindi ‘ kiduchu’. Kufunga magoli ni wajibu wa kila mchezaji ndani ya uwanja, ila goli halipatikani bila mipango. Ni namna gani, Stars itaweza kuuvunja ukuta  ambao ukitoa wachezaji wanaocheza nje, ulikuwa mgumu sana katika CHAN 2014?

640_340_Knowledge-Musona-chiefsKnowledge Musoma

Majibu anayo kocha, Nooij, ila itakuwa si makosa kuwakumbusha washambuliaji wa Stars kuwa makini na kila nafasi inayopatikana katika kufunga magoli ya kutosha. Mpira hauwezi kuingia golini bila ‘ kupigwa’, ni lazima kujitahidi kupiga mipira mingi katika lango la The Warrios. Mfumo wa 4-3-3 ungeweza kusaidia kwa kuwa ni rahisi kuuvunja ukuta wa walinzi wanne, ila Stars haina wachezaji wa kucheza katika mfumo huo kwa usahihi kama haina washambuliaji, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

SAFU YA KIUNGO… Salum Abubakary, Frank Domayo, Saimon Msuva, na Himid Mao, kwa pamoja wanastahili kuanza katika nafasi ya kiungo ya Stars. Kwa, nini nasema hivyo?. Hii ni mechi ya mtoano, bila kufunga magoli timu inakuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele, lakini unaporuhusu goli/ magoli katika mchezo wa kwanza tena ukicheza katika uwanja wa nyumbani itakuwa ni ‘ miujiza’ kushinda ugenini.

Katika uwanja unaochukua watazamaji, 60, 000, jijini, Harare, Stars haitakiwi kwenda katika mchezo wa marejeano ikiwa imeruhusu goli katika uwanja wa Taifa, jumapili hii. Sababu kubwa ya kuwahitaji viungo hawa ni viwango vyao, namna wanavyopokea maelekezo ya wakimu na kuyafinyia kazi, wanavyowajibika mchezoni, na haina ya wachezaji tunaokwenda kukutana nao.

Stars inahitaji magoli, ila haipaswi kufunguka sana uwanjani ili kutofungwa. Salum, ni kiungo mzuri wa mashambulizi akitokea katikati ya uwanja, ana pumzi ya kutosha, mpigaji mzuri wa pasi, kama atarekebisha tatizo lake la kupiga pasi nyingi za pembeni na kuzipiga kwa washambuliaji wa kati itakuwa jambo lenye faida kwa timu. Himid ni mzuri katika ukabaji, kama ilivyo kwa Salum, naye pia ni mchezaji mwenye kucheza kwa nguvu uwanjani, anaweza kucheza upande wa kulia, kushoto au kiungo wa kati.

Wakati, Zimbabwe, ikimtumia zaidi mkongwe, Dany Phin, 34 ambaye ametokea kuwa mchezaji muhimu wa safu ya kiungo ya timu hiyo tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwaka huu, wanaye Ali Sadiki, 26, katika wingi ya kushoto. Mchezaji huyo anayecheza katika klabu ya Platim pamoja na mkinzi, Gift Belo, ni hatari katika mashambulizi hivyo, ukiachana na uwepo wa Frank Domayo katika nafasi kiungo-mlinzi, Himid atahitajika ili kuifanya Stars kuwa na nguvu katikati ya uwanja kwea muda wote.

Sadiki, mameshaiwakilisha Zimbabwe mara 11 hivyo ni mmoja kati ya wachezaji wa kuchungwa sana uwanjani. Willard Katsande, 28 ndiye kiungo wa mashambulizi wa Zimbabwe, ambaye katika michezo 13 aliyoiwakilisha nchi yake amefanikiwa kufunga magoli mawili. Domayo atakuwa na jukumu la kumchunga na kumzima kiungo huyo wa klabu ya Kaizer Chief.

33ef2ee24799a0634c84a94a65e44994Peter Moyo, 26 mchezaji wa klabu ya Highlanders, pia ni hatari katika kupiga pasi za mwisho. Kocha, Ian hupendelea kuwapanga kwa wakati mmoja, Phin, Katsande, Sadiki, na Moyo. Tutahitaji kuona, Msuva akikimbia na mipira na kupiga krosi sahihi kwa washambuliaji wa kati.
Msuva, ni mwepesi na mchezaji mwenye kasi hivyo kuwepo kwake uwanjani kutafanya, Domayo ambaye japo hucheza zaidi nyuma ni mtaalamu wa pasi za mbali. Wachezaji hawa wote ni vijana hivyo ni wakati wa kuwaamini na wao kuthibitisha ubora wao kwa kuisaidia Tanzania kupata ushindi.

SAFU YA ULINZI; Wakati mchezaji mwenye umri mkubwa katika kikosi cha Zimbabwe akiwa ni kiungo wa ulinzi, Phin ambaye amecheza michezo 11 tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mapema mwaka huu, Stars itakuwa na mlinzi na nahodha mpya wa timu hiyo, Nadir Haroub, 32. Nadir amekuwa mchezaji wa timu ya Taifa tangu mwaka, 2006 atakuwa na jukumu kubwa la kumuongoza, Aggrey Morris, kuwazima washambuli-pacha, Knowledge Musona, 23, na Kingston Nkhatha ambao wanaichezea klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

Musona, nahodha wa kikosi hicho tayari amefunga magoli 12 katika michezo 19 aliyoiwakilisha nchi yake, wakati Kingston amefunga magoli
mawili katika michezo 10. Kama, Stars itaweza kuwazima viungo, Sadiki, Moyo na Katsande kamwe hutaona uwezo wa washambuliaji hao, ila kama The Warrios watapata muda wa kumiliki mchezo kwa dakika walau 15, Musona na Kingston ni wachezaji wanaweza kutuzamisha na kwenda, National Sports Stadium tukiwa na nafasi ndogo. Shomari Kapombe, Oscar Joshua hawapaswi kupanda mara kwa mara, wawe makini zaidi kuhakikisha timu haruhusu goli/magoli.

Mara nyingi timu zetu zimekuwa zikifungwa magoli katika dakika za mwanzo, hiyo ni dalili ya timu kukosa umakini. Je, tunapaswa kuendelea kufungwa na kuondolewa katika michuano ya kimataifa?. Hii inaweza kuwa nafasi yetu, lakini ni kwa kupambana. Udhamini wa dola millioni mbili uendane na matarajio ya muda mfupi ya timu yetu ya Taifa. Sasa ni wakati wa wachezaji kucheza soka huku wakionekana wamepevuka, wana hamu ya kufuzu kwa michuano ya Afrika. Lolote linaweza kutokea kama tutafuzu kwa hatua ya makundi. Tunaiunga mkono, Taifa Stars, ni wakati wa wachezaji wetu kucheza soka la matokeo. Nimewasilisha tu.

0714 08 43 08

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here