Home Makala TUNATAKA NYUMBA IMARA KWA MSINGI WA UDONGO MFINYANZI

TUNATAKA NYUMBA IMARA KWA MSINGI WA UDONGO MFINYANZI

1352
0
SHARE

20140502_111547Nilipokua mwanafunzi wa shule ya msingi sikuwahi ona umuhimu wake mpaka nilipo hitimu.Ungeniuliza kipindi hicho kwanini nasoma shule ya msingi,Nisingekua na jibu la kukupa.Nilikua nikiona kama utaratibu fulani wa ukuaji wa mwanadamu. Sikuwahi kufikiria kua siku moja elimu ya shule ya msingi itanisaidia.Ilinichukua miaka saba tu kugundua siri iliyofichika ndani ya elimu ya msingi.
Ilikua kazi nyepesi sana kukabiliana na masomo yangu ya sekondari kutokanana msingi imara niliotoka nao shule ya msingi,sikuhitaji nguvu nyingi kwenda sambamba na masomo ya sekondari, na siri kubwa ilikua ni msingi imara nilioupata shule ya msingi.
Kila kitu bora huanza kwa msingi imara.
Ndugu yangu mwashi neno msingi si neno geni kwake,Nyumba bora hujengwa kwenye msingi imara.Hata nyumba yenye wagivu kwa rangi nzuri,bila msingi imara haiwezi kua nyumba bora.Ila nyumba bora hukamilika kwa msingi imara.Nyumba imara hujengwa juu ya mwamba kama si nondo nzito zinazoambatana na kokoto makini.Vitu vyote hivi bora na imara huambatana sambamba na muda bila kusahau gharama pia.
Kwa wale wenye haraka ya kuukimbia muda na kukwepa gharama hutumia changarawe sambamba na udongo mfinyanzi kama mbadala wa kokoto ,Na matokeo yake baada ya kusimamisha jengo wanaingia gharama za kuziba nyufa kila wakati na mwisho wa siku nyumba hiyo haidumu. Mwenye hekima atajenga nyumba yake juu ya mwamba imara na kudumu nayo milele ila mpumbavu atajenga kwa changarawe na kukaa nayo kwa miaka miwili kabla ya kujenga nyingine.
Waafrika wengi hasa Watanzania tunapenda vitu vya harakahara na vya bei chee.Tunajali sana kumaliza kuliko kufanikisha.Kwenye kila sekta tumetawaliwa na pupa zinazopelekea tusifanikiwe.
Ebu nitoe king’ong’o nitumie mdomo kusema kitu juu ya soka la bongo.Kila siku tumekua watu wenye kiu ya kufanikiwa lakini tunaishia kuwa wahasidi.Tumekua kama wapumbavu tunaotaka mambo mazuri bila kufa kidogo. Tumekua na husuda pasi nakujifunza.Kila siku tunasoma na kuona nchi zilizoendelea kisoka zimefanya nini mpaka zimefika zilipo lakini hatutaki kujifunza katika mifano hiyo. Tumefumbwa macho kwa ujinga kusubiri bahati nasibu.
Mwaka jana mwezi wa sita nilipata bahati kushuhudia baadhi ya mechi za umitashumta mjini kibaha.Nilijionea hazina kubwa inayoenda kuliwa na tunutu.Bahati nzuri nzuri nilipata kuongea na kocha wa timu ya taifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 15,Kocha huyo alisema “tatizo la wachezaji wa Tanzania hawapati nafasi ya kukaa muda mrefu kwa pamoja tangu wakiwa na umri mdogo, utakuta mtoto wa kwetu wa Denmark na wa Tanzania wana vipaji sawa ila tofauti yetu inakuja onekana sababu ya wachezaji wetu kukakaa kwa muda mrefu kwenye akademi za soka na kujifunza kucheza kitimu zaidi” hapo kocha huyo alimaanisha kua Tanzania wanahitaji kujenga msingi imara wa soka kwa kuanzia kwenye akademi za soka.
Maneno ya kocha huyo ni ukweli mtupu,huwa sitaki kuamini kama wachezaji wa ulaya wana vipaji vya ajabu ukilinganisha na wakwetu Afrika.Tofauti yetu ni jinsi ya kutunza na kuendeleza vipaji hivyo.Sammata angezaliwa Uingereza angekua anachezea Manchester united wakati welbeck angezaliwa Tanzania angekua anachezea Tp mazembe.Hapo kilichobadilika ni mahali mchezaji husika alipozaliwa tu.wakati welbeck tangu akiwa na umri wa miaka 11 akilelewa kwenye akademi za soka za Manchester united,sammata bila shaka alikua akizunguka huku na kule na sembo mkononi kujaribu bahati yake mitaani.Hili ni tatizo.Samaki mkunje angali mbichi,mchezaji mzuri hufunzwa tangu utotoni.Inatubidi kua wavumilivu,tunahitaji kujitoa kwa muda na gharama pia
Nikisema gharama utaniambia nchi yetu ni maskini,Lakini kuna nchi masikini kama Tanzania tena nyingine ni masikini zaidi ya Tanzania lakini zimepiga hatua kubwa katika soka kuliko Tanzania.Angola ni moja ya nchi maskini kuliko Tanzania lakini pamoja na umaskini wao wamewai shiriki Kombe la Dunia huku Tanzania ikiangaika kila siku kutafuta japo nafasi ya kushiriki AFCON bila mafanikio yeyote.
Nikikwambia muda utachoka kusubiri huku ukiwaza kwenda Brazil kwa kambi ya wiki mbili wakati wengine waliandaa timu ya kombe la Dunia miaka 10 iliyopita.Hapa hatuna ujanja zaidi ya kuwa wavumilivu,Senegal walivumilia wakaweza,Spain walivumilia wakafanikiwa.Hakuna mchezaji hata mmoja wa kikosi cha kwanza wa timu ya taifa ya spain ambaye hajapitia shule za mafunzo ya soka.Na kikubwa zaidi hakuna hata mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha spain ambaye hajapitia timu ya taifa ya vijana.Andres iniesta ambaye ni moyo wa timu hiyo amechezea timu za vijana za madaraja yote tangu akiwa na umri wa chini ya miaka 11
Nashukuru kwa maono mapya ya Tff kuunda Timu ya taifa upya.Imethubutu kuzunguka kila mkoa kusaka vijana wenye vipaji waliounda timu ya taifa mpya.Sina uhakika kama ni utaratibu mzuri wametumia,sina uhakika kama mchezaji mzuri anatafutwa kwa njia walizotumia,Ila nina uhakika wachezaji hao hawatoleta mabadiliko kwenye soka letu.
Wengi wao watakua wale wale aliosema kocha wa vijana.Hatuhitaji kuruka hatua yeyote,tunahitaji kwenda ngazi kwa ngazi.Ili kujenga timu imara tunahitaji kuanzia kwa wachezaji wanaotoka umitashumta
Umitashumta itatupeleka kombe la Dunia kama sio Mataifa ya Afrika.Tuache mipango yetu mifupi ya zimamoto na kuandaa mipango ya miaka nane ijayo.
Malinzi na Tff yake isifikiri kupata mafanikio makubwa kwa muda waliopewa.Malinzi na TFF kwa ujumla inabidi itujengee msingi Imara kupitia kutunza na kuendeleza vipaji vinavyopatikana umitashumta.
Kama vijana hao ambao wengi ni chini ya umri wa miaka 15 watatunzwa na kuendelezwa tutaongea mengine baada ya miaka nane.Tff inabidi iwekeze zaidi kwenye umitashumta ili kujenga msingi imara wa soka la Tanzania kwa miaka mingi ijayo.

Imeandikwa na
Kaijage jr(middle ya juu)
kaijagejr@gmail .com,0655106767

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here